Picha : KIKAO CHA WADAU WA ELIMU MKOA WA SHINYANGA


Hapa ni katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo leo Jumatano Julai 19,2017 kunafanyika kikao cha wadau wa elimu mkoa wa Shinyanga. Kikao hicho kinaongozwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela.



Kikao hicho pamoja na mambo mengine kinalenga kujadili mafanikio na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu mkoani Shinyanga.Miongoni mwa mambo yaliyoleta mjadala mrefu zaidi ni pamoja na suala la mimba kwa wanafunzi na uhaba wa vyoo katika shule.


Mwandishi wetu Kadama Malunde,yupo katika kikao hicho ametuletea picha za matukio yanayojiri katika kikao hicho..Tazama Hapa chini

Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi akizungumza wakati wa kikao hicho ambapo alisema idadi ya wanafunzi na usajili wa shule mpya umeongezeka mkoani Shinyanga wakati wa mfumo wa elimu bila malipo.

Katibu tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akizungumza ukumbini ambapo alisema ili kumaliza changamoto zilizopo katika sekta ya elimu ni vyema wadau wote wakashiriki katika kutatua changamoto hizo.

Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini

Wadau wa elimu wakiwa ukumbini.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akichangia hoja wakati wa kikao hicho.

Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya mkoani Shinyanga wakiwa ukumbini

Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini

Wadau wakiwa ukumbini

Kikao kinaendelea

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu,Boniface Butondo akichangia hoja wakati wa kikao hicho.

Mchungaji Joram wa kanisa la Waadventista Wasabato mjini Shinyanga akichangia hoja ukumbini.

Kikao kinaendelea

Mdau akichangia hoja ukumbini

Kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngassa Mboje na Diwani wa kata ya Kambarage mjini Shinyanga,Hassan Mwendapole wakisoma nyaraka muhimu wakati wa kikao hicho.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Simon Berege akichangia hoja ukumbini

Wa kwanza kushoto ni Padre Joachim Mahona kutoka kanisa katoliki Jimbo la Shinyanga na Mwenyekiti wa makanisa ya kipentekoste mkoa wa Shinyanga Mchungaji Elias Madoshi kutoka kanisa la FPCT wakisoma taarifa muhimu ukumbini.

Kikao kinaendelea..

Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi akisoma taarifa wakati wa kikao hicho


Kushoto ni katibu tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akitafakari jambo ukumbini







Powered by Blogger.