Mwanza: Mwalimu Afumaniwa Akifanya Mapenzi na Mwanafunzi Wake Darasani
Mwalimu
Abasi Hussein wa shule ya msingi Mwabomba iliyopo tarafa ya Ngula
wilayani Kwimba mkoani Mwanza anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma
za kukutwa darasani akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha nne
mwenye umri wa miaka 17.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo mkoani humo na kusema mpaka sasa mwalimu huyo mwenye umri wa miaka
27 anashikiliwa na jeshi la polisi muda wowote upelelezi ukikamilika
mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
"Babu
wa mwanafunzi alipoona mjukuu wake amechelewa kurudi nyumbani alianza
kufanya msako, alikwenda kwenye shule ya sekondari lakini hakumuona
ikabidi aendelee kumtafuta mjukuu wake, ilipofika kwenye muda wa saa
sita na kitu alikwenda kwenye shule ya msingi ya Mabomba katika moja ya
darasa wakakuta huyo mwanafunzi wa kike akifanya mapenzi na mwalimu wa
shule hiyo ya msingi ya Mwabomba" alisema RPC Msangi
Msangi aliendelea kuelezea jinsi babu alivyoweza kuwakamata watu hao
"Yule
babu alikuwa ameongozana na watu wengine hivyo walipowaona waliwakamata
wakaita na watu wengine, baadaye taarifa zilifika kituo cha polisi na
polisi walikwenda na kuwakuta watuhumiwa hao kwenye lile darasa hivyo
wakawachukua na kuwafikisha kituoni, hivyo mtuhumiwa yupo kituo cha
polisi tunaendelea na mahojiano na taratibu nyingine za kiupelelezi
zinaendelea ili tuweze kukamilisha upelelezi tuweze kumfikisha
mahakamani kujibu tuhuma hizo" alisisitiza Msangi
Mbali
na hilo Kamanda Msangi ametoa onyo kwa watu wanaojihusisha na mapenzi
na watoto chini ya miaka 17 na kusema huenda awe amekubali mwenyewe hilo
ni kosa la ubakaji hivyo amewataka kuacha na kusema kufanya vitendo
hivyo ni sawa na kuhitaji kwenda jela miaka 30.