MKAPA AWATAKA VIONGOZI KUBUNI MIRADI ILI WANANCHI WANUFAIKE.
Rais Mtaafu wa awamu ya
tatu Benjamini Mkapa akipata maelelzo toka kwa mtaalamu wa wa afya jinsi kituo
hicho kitakavyotoa huduma kwa wananchi mara baada ya kufungua jengo la upasuaji
katika kituo cha afya nkoma wilayani itilima mkoani simiyu.
Rais wa awamu ya Tatu Benjamini mkapa akikagua vitanda ndani ya jengo la upasuaji baada ya ufunguzi wake katika kituo cha Afya nkoma wilayani Itilima mkoani Simiyu leo.
Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga akiongea na wananchi wa kata ya Nkoma baada ya ufunguzi wa jengo la upasuajia katika kituo cha afya nkoma
Rais
Mstaafu Benjamini Mkapa akimkabidhi cheti/hati ya jengo la upasuaji Mwenyekiti
wa halmashauri ya Itilima Daudi nyalamu kwa niaba ya Halmashauri hiyo
lililojengwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa.
|
Rais wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa akiwahutubia wananchi wa kata ya nkoma mara baada ya kukabidhi jengo la upasuaji kituo cha afya nkoma lililojengwa na taasisi yake |
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kata ya nkoma katika hafla ya kukabidhi jengo la upasuaji lililojengwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa. |
Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
RAIS wa Awamu ya tatu Benjamini
mkapa amekabidhi jengo la upasuaji na kuwataka watanzania kujitegemea katika
kubuni miradi ambayo itasadia jamii kwa lengo kuondokana na utegemezi wa
mataifa tajiri .
Mkapa amesema kuwa kama taifa
tusitarajie mataifa tajiri kuja kutuinua kama sisi wenyewe tumekaa kwa kuwa
hiyo ni dhana potofu inayorudisha nyuma juhudi za maendeleo kwa wananchi.
Rais Mkapa ameyasema hayo wakati
akifungua jengo la upasuaji katika kata ya Nkoma wilayani Itilima mkoani Simiyu
huku akiwasisitiza viongozi wa serikali kubuni miradi ili kujiendeleza kama
wanavyofanya nchi ya Japan.
Jengo hilo ambalo limejengwa na
taasisi ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na nchi ya Japan limegharimu
milioni 270 ambapo wakinamama wajawazito, watoto na wagonjwa walikuwa wakiipata
huduma hiyo umbali wa kilomita 40.
Alisema kuwa mijadala mingi
inayoendelea kwa sasa ni ya kisiasa na siyo ya kuleta maendeleo hivyo jamii na
taifa kwa ujumla wanao wajibu wa kuongeza ari katika kujiendeleza na
kujitegemea kwa wasomi, wananchi na wafanyakazi.
Aliongeza kuwa kila mtanzania ana
wajibu wa kuhakikisha taifa linajitegemea na kuwaletea wananchi wake maendeleo,
huku akiwataka wasomi na wafanyakazi kuendesha midahalo na makongamano ya
kuhakikisha nchi inajitemegea.
“ kila siku utasikia watu wanadai
haki, makongamano, midahara ya kudai haki, swali la kuwauliza wao je wametimiza
wajibu kama watanzania? Maana hakuna haki bila wajibu, ni lazima kubadilika na
kuendesha makongamano ya kuonyesha nchi itajitegemea vipi” alisema Mkapa.
Aidha aliongeza kuwa ili kuweza
kujitegemea ni lazima kila mtanzania akatimiza wajibu wa kufanya kazi kama Rais
Magufuli anavyosema, huku akitoa mfano katika nchi ya Japani kuwa wananchi wake
jambo la kwanza ni kufanya kazi.
“ kama tunatarajia mataifa kuja
kutuinua wakati sisi tumekaa, ni dhana potofu, vuongozi tubuni miradi ili
tujiendeleze na kujiletea maendeleo sisi wenyewe, kaama nchi ya Japani
wanavyofanya” alisema Mkapa.
Aliongeza kuwa toka utawala wa Baba
wa Taifa na sera ya Chama cha Mapinduzi toka zamani ilikuwa ujamaa na
kujitegemea, jambo ambalo ameeleza lazima yatekelezwe kwa kila mmoja katika
kutimiza wajibu kwa nafasi yake.
Akiongelea Jengo hilo Mkapa
ameishukuru nchi ya Japana ambao walitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo
hilo kupitia taasisi ya Mkapa foundation, huku lengo likiwa kupunguza vifo vya
akina mama wajawazito na watoto wachanga.
“ Nchi yetu bado tunakabiliwa na
changamoto ya vifo vya akina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga, Nchi ya
Japan wametoa msaada huo kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hii, taasisi ya
Mkapa foundation itaendeleza ushirikiano na serikali katika kutatua changamoto
mbalimbali za afya” alisema Mkapa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa vifo vitokanavyo na uzazi
kati ya wakina mama 100,000 vimepungua kwa mwaka hadi 559 kwa mwaka ambavyo
husababishwa na kuvuja damu, maambukizi ya maradhi na uzazi pingamizi.
Mwalimu alisema kuwa serikali
itaendelea kutatua changamoto za afya hasa huduma ya upasuaji ili kufuikia 2020
angalau 50% ya vituo vitoe huduma ya upasuaji ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
Alisema kuwa kufikia mwezi Desemba
mwaka huu katika jengo hilo serikali italeta mashine ya ultra sound ili kuweza
kukidhi mahitaji ya wagonjwa, na pia wataajiri zaidi ya watumishi wa afya 3000
na kupunguza changamoto ya uhaba wa watumishi wa afya.
Katika hatua nyingine Mwalimu
amesema kuwa serikali imetoa bei elekezi kwa dawa za binadamu ili hata
mwananchi mwenye kipato kidogo aweze kumudu gharama za matibabu huku
akisisitiza kuwa dawa siyo bure.
‘’bei za dawa siyo bure na wananchi
mnatakiwa kuchangia dawa katika vituo na zahanati…bei za dawa zimepunguzwa
tangu jana na tunataka wananchi waone upungufu huo katika madawa ya kupata dawa
hizo’’ alisema Mwalimu
Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga
alisema kuwa pamoja na kukamilika kwa jengo hilo upungufu wa watumishi bado ni
changamoto kubwa wajibu wa serikali ni kuajiri watumishi ili waeze kuhudumia
wananchi.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria
katika ufunguzi huo walisema kuwa jengo hili limeongeza faraja kwa akinamama
wajawazito na wagonjwa kwani wengi wao walikuwa wakifia njiani wakati
wakisafirishwa kwenda Bariadi kupata huduma ya upasuji.
Mary Kasuka mkazi wa Mwalushu
alisema kuwa awali walikuwa wakipata taabu sana kupata huduma ya upasuaji na
wanaishukuru taasisi hiyo kwa kuwasogezea huduma ya upasuaji na kuitaka
serikali kuhakikisha huduma ya maji inapatikana wakati wote kituoni hapo.