MAKABURI MATANO YA WATU WENYE VIPARA YAFUKULIWA....INADAIWA WENYE VIPARA WANA DHAHABU KICHWANI
Wakazi wanaoshi katika wilaya ya kati ya
Milange nchini Msumbiji wanasema kuwa miili ya watu watano wenye vipara
imefukuliwa katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na masuala ya
uchawi.
Watu wanaamini kwamba mwili wa mtu mwenye kipara una dhahabu , kulingana
na kamanda mmoja wa polisi kwa jina Afonso Dias alieambia BBC mnamo
mwezi Juni baada ya misururu ya muaji iliolenga watu wenye vipara.
Wakaazi wa Milange wameitaka serikali kuingilia kati.
Kufikia sasa wakaazi ,na watumiaji wa dawa za kitamaduni pamoja na
waliopigania uhuru wamekutana na maafisa wa taasisi ya kitaifa ya urithi
na usaidizi wa haki IPAJ.
Mwakilishi wa IPAJ Antonio Gussi aliahidi kuwasilisha malalamishi yao
kwa mamlaka husika ,lakini pia akawataka kutokubali tamaduni hizo
zilizopitwa na wakati katika siku za usoni.
Chanzo-BBC