KAMPUNI YA GRUMETI RESERVES LTD WALIPA ZAIDI YA SHILINGI BILLION 1. 3 JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI IKONA WMA

Meneja
Mahusiano wa Kampuni ya Grumeti Reserves Ltd Ami Seki kulia akimkabidhi
Mwenyekiti wa Ikona Wma Elias Nchama kushoto Hundi ya zaidi ya sh Bill
1.3 ikiwa ni malipo ya deni za miaka mitatu walilokuwa wanadaiwa na
Jumuiya hiyo ya Uhifadhi,ikiwa ni gharama za pango,ushuru wa
Vitanda,Upigaji Picha na uwindaji wa kitalii.




Hata
hivyo baada ya makabidhiano hayo Meneja mahusiano wa kampuni ya Grumeti
Ami Seki ametoa shukrani zake huku mwenyekiti wa IKONA WMA Elias Nchama
akitumia fursa hiyo kuomba radhi pale ambapo wamekwazana katika kudai
malipo hayo na kusema sasa yataenda kutekelza miradi ya wanachi
ilikusudiwa.



"Naomba mkafikishe
ujumbe kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Grumeti pale ambapo tumekosea naomba
radhi kwa niaba ya wajumbe wote wa IKONA WMA" alisema Elias.

Katibu
wa Ikona Wma Yusuph Manyanda kulia akisaini makubaliano ya hiyari kati
ya Jumuiya hiyo na Kampuni ya Grumeti Reserves Ltd ambayo yanawapa
wajibu pande zote za kuheshimu taratibu za uwekezaji na uhifadhi,kushoto
ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Elias Nchama.


Mwenyekiti wa Ikona Wma Elias Nchama akisaini Makubaliano ya hiari ,kushoto ni Katibu wa Jumuiya hiyo Yusuph Manyanda.


Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Grumeti Reserves Ltd Ami Seki akisaini
makubaliano ya hiari kati yao na Ikona ,kulia kwake ni Msaidizi wake
David Mwakipesele.

Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Simioni
Warioba kushoto na Afisa wanyamapori wilaya hiyo John Lendoyan wakisaini
makubaliano ya hiari kati ya Grumeti Reserves na Ikona Wma.



Wakili Maganiko Msabi ambaye ni Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya
Serengeti akitoa maelekezo kabla ya kusaini makubaliano ya hiayo ya
kampuni ya Grumeti Reserves na Ikona Wma.


Katibu wa Ikona Wma Yusuph Manyanda akitoa ufafanuzi wa pesa
zinazotakiwa kulipwa na Grumeti Reserves kabla ya kusainiana makubaliano
ya hiari.

      Hundi ya Mfano ikikabidhiwa kwa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanayamapori IKONA (WMA)

                      Wajumbe wa Bodi ya Ikona na wajumbe wa baraza la Jumuiya hiyo wakifuatilia



                   Wanasheria  wa pande zote mbili kwa upande wa serikali na kampuni ya Grumeti wakielekeza jinsi ya kujaza maridhiano hayo.

              TAZAMA VIDEO HAPA CHINI UPATE HABARI KAMILI JUU YA TUKIO HILO


Powered by Blogger.