Kamanda Mpinga Ang’olewa Usalama Barabarani.....Apelekwa Kuwa RPC Mbeya
IGP
Sirro, amefanya mabadiliko katika jeshi la polisi ili kuboresha
utendaji wa jeshi hilo kwa kumuhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi
Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Mohamed
Mpinga na kuwa Kamanda wa polisi wa mkoa Mbeya
Katika
taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi inasema kuwa aliyekuwa Kamanda
wa polisi mkoa wa Mbeya (DCP) Dhahiri Kidavashari amehamishiwa Makao
Makuu ya upelelezi.
Kufuatia
mabadiliko hayo nafasi aliyokuwa nayo Mohamed Mpinga imechukuliwa na
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu.
Kwa
mujibu wa Barnabas Mwakalukwa (ACP) ambaye ni msemaji wa jeshi la
polisi, Makao Makuu ya Jeshi hilo amesema uhamisho huo ni wa kawaida
katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni,
taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
IGP
Saimon Sirro alishauriwa na Rais John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko
katika jeshi hilo ili kuleta ufanisi na kuboresha utendaji wa jeshi la
polisi nchini, jambo ambalo tayari inaonyesha ameanza kulifanyia kazi
kwa kufanya mabadiliko kama haya.