Isome hapa hati ya shtaka alilosomewa Tundu Lissu mahakamani na Kisha Kunyimwa Dhamana
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana alisomewa mashtaka ya uchochezi na kurudishwa rumande akisubiri hatma ya dhamana yake.
Lissu alisomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbert Mashauri.
Mawakili
watano wa upande wa Jamhuri waloshiriki katika kesi hiyo, waliiambia
Mahakama kuwa Lissu alitenda kosa hilo la jinai Julai 17 mwaka huu
katika eneo la Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Lissu
ambaye alikuwa akitetewa na jopo la mawakili 20 wakiongozwa na Fatma
Karume, alikana mashtaka dhidi yake. Mbunge huyo pia alisikika akisema,
“kwakweli halijawahi kuwa kosa la jinai.”
