BAADA YA KUMTOSA MINGANGE, NDANDA FC YASAKA KOCHA NJE YA TANZANIA
Baada ya kuachana na Kocha Abdul Mingange, klabu ya Ndanda FC imeanza mazungumzo na makocha wawili kutoka nje ya Tanzania.
Taarifa zinaeleza, Ndanda FC imeamua kujiimarisha zaidi katika benchi la ufundi kwa kupata kocha kutoka nje ya Tanzania.
Msemaji wa Ndanda FC, Iddrisa Bandari amethibitisha kuwa wanataka kocha kutoka nje ya Tanzania.
“Ni
kweli tunazungumza na kocha ambaye atatoka nje ya Tanzania. Lakini kwa
sasa mazungumzo hayajakamilika ndiyo maana hatuwezi kusema jambo,”
alisema.
Mingane alirejea Ndanda FC akitokea Mbeya City na kuisaidia kutoteremka daraja lakiniinaonekana ameshindwa kudumu tena.