Picha katika matukio Afisa Tawala Mwandamizi Halmashauri ya Mji wa Tarime Mwita Laurent Marwa kusimamishwa kazi kwa kusababishia taasisi za kifedha hasara ya Shilingi Milli0n 28 na watumishi 60 kupewa siku tatu za kujieleza


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa akiongea na watumishi wa Halmashauri hiyo na kulaani Vikali kitendo cha Afisa Tawala Mwandamizi Mwita Laurent Marwa kwa kisababishia Taasisi za kifedha hasara ya Shilingi Millioni 28 kutokana  na udanganyifu ambao amekuwa akiufanya kwa kushirikiana na Watumishi huku silimia 90 wakiwa ni Walimu. wakati wa kuchukua na kurejesha Mikopo 


"Serikali ya sasa hivi haitaweza kufumbia macho suala hili watumishi tulishawasomea waraka huu kuhusu taratibu za kufuata katika kuchukua mikopo mimi ndiye mwenye dhamna lakini bado wengine wanachukua mikopo bila taratibu sasa kama huyo amekuwa akibadili mtu akichukua mkopo wa millioni kumi na tano mfano kama anapaswa arejeshe laki mbili na na Eftu tano sasa anakata hizo fedha na kuweka senti au shilingi elfu moja ndo zinasomeka kwenye mfumo na laki mbili  zinabaki na baada ya muda anaonekana kamiliza mkopo na kuenda kukopa sehemu nyingine kuanzia sasa namsimamisha kazi tutaendelea kuchunguza kwa siku 14 na hawa 60 nawapa siku tatu za kujieleza nao tutawachukulia hatua kali" alisema Elias.



Watumishi wote wa Halmashauri ya Mji wa Tarime wakisikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Elias Ntiruhungwa  ambapo amewataka kuondokana na tamaa za kimaisha bali wafuate maadili ya kiutumishi



Mkurugenzi wa Halamashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa akionesha majina 60 ya baadhi ya watumishi wakiwemo Walimu ambao wamekuwa wakishirikiana na Afisa Utumishi kufanya udanganyifu wa kifedha katika kurejesho Mikopo ya Taasisi za kifedha mbalimbali na kusababisha hasara ya shiringi millioni 28



Afisa Mipanga Halmashauri ya Mji wa Tarime Belton Garigo akisisitiza watumishi hao kuendelea kusimamia vyema miradi inayotekelezwa na serikali ikiwemoi Elimu, Afya, Maji na Barabara.


Kaimu Afisa Utumishi Jonia Kafuruki akisistiza suala la maadili ya Utumishi kwa watumishi hao ambapo amewataka watumishi hao kufuata kanuni na taratibu katika sula zima la kwenda masomoni na upatukanaji wa ruhusa


Powered by Blogger.