VIDEO: MAIRO MFANYABIASHARA TARIME ASAIDIA WALEMAVU WA NGOZI NA VIUONGO




Mfanyabiashara
na Mmiliki wa MAIRO Filling Station Mairo Marwa Wansako kushoto
akikabidhi Baiskel yenye thamani ya shilingi Laki Nne kijana aitwaye
Matiko Marwa Mkazi wa Mtaa wa Itebe Kata ya Nkende Halmashauri ya Mji wa
Tarime ambaye pia ni Mwanafunzi wa Darasa la Tatu Angel House aliyekaa
kwenye Pikipiki ni Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wilayani
Tarime CHAWATA Yohana Kemweneti.

Mairo amesema kuwa ameamua
kusaidia kijana huyo baada ya kuona ameteseka kwa muda mrefu ili usafiri
huo atumie akiwa shuleni jambo ambalo linaweza kuwa chachu ya ufaulu
ili kutimiza ndoto zake

"Nimekuwa nikisaidia watu wengi wakiwemo
walemavu wa Ngozi Albino hata juzi nimesaidia Msichana aitwaye Sala ni
Mlemavu wa Macho ili aweze kwenda shule" alisema Mairo.

Matiko
Marwa Mkazi wa Mtaa wa Itebe Kata ya Nkende Halmashauri ya Mji wa
Tarime ambaye pia ni Mwanafunzi wa Darasa la Tatu Angel House akiongea
na CLEO24 NEWS Baada ya kupewa msaada wa Baiskeli

Sala
Marwa mkazi wa mtaa wa Songambele A Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani
Mara akiongea na CLEO24 NEWS huku akitaja changamoto zinazowakabili
watu wenye ulemavu wa Viungo na kuiomba serikali na jamii kwa ujumla
kuendelea kuwasaidia ili kutuimiza ndoto zao.

Mwenyekiti
wa chama cha watu wenye ulemavu CHAWATA Tarime Yohana Kemweneti
akiongea na CLEO24NEWS Kuhusu changamoto zinazowakabiri walemavu ambao
amepongeza jitiahada za serikali na kuiomab kuendelea kuwakumbuka
hususani marneo ya Vijijimni na kuwaomba wazazi na walezi kuondokana na
suala la kuwaficha watu wenye ulemavu bali wapelekwe shule ili kuweza
kutimiza ndoto zao.
                                          TAZAMA VIDEO CHINI


Powered by Blogger.