Video, Picha: Katika Matukio tofauti ATFGM Masanga watumia Michezo siku ya Mtoto wa Afrika kufikisha Elimu yak up[iga Vita Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike ,kulinda na Kutetea haki za watoto Mkoa wa Mara.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika viwanja vya shule ya Msingi Masanga Mwl Ryoba Mariba ambaye ni Afisa Taaluma kwa niaba ya Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini akionesha moja ya kombe ambalo litazawadiwa washindi wa soka kati ya timu za sekondari na Msingi zilizoshiriki kwenye mashindano yaliyoandaliwa na ATFGM Masanga kwa lengo la kufikisha Elimu ya kupiga vita ukatili wa kijinsia na ukiukaji wa haki za watoto.
Kikundi cha GALAX wakitoa elimu juu ya madhala ya Ndoa za utotoni kupitia Maigizo katika Maadhimisho hayo yaliyofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Masanga baada ya kuandaliwa na ATFGM Masanga kwa kushirikiana na Shirika la RIGHT TO PLAY
Leah Kimaro Msimamizi wa Mradi wa kupiga Vita ukatili wa Kijinsia na kutetea haki za Watoto kutoka Shirika la RIGHT TO PLAY akieleza siku ya Mtoto wa Afrika na ni jinsi gani watoto wa kiafrika walibaguliwa huko Afrika kusini na kuamua kuingia barabarani kwa lengo la kudai haki zao.
Stephen Ngonyani Mratibu wa Klabu za Haki za Watoto ATFGM Masanga akieleza umhimu wa Michezo katika Siku ya Mtoto wa Afrika
Watoto wakikimbia kwenye Magunia
Mchezo wa kuvutana na kamba
Watoto wakikimbia Mita 100
Watoto wakikimbiza Kuku
Watoto wakijibu Maswali
Leah Kimaro Msimamizi wa Mradi wa kupiga Vita ukatili wa Kijinsia na kutetea haki za Watoto kutoka Shirika la RIGHT TO PLAY akiongea na Vyombo vya Habari juu ya watoto kutumikishwa katika maeneo mbalimbali
Stephen Ngonyani Mratibu wa Klabu za Haki za Watoto ATFGM Masanga akiongea na vyombo vya habari kuhusu umhimu wa Michezo katika Siku ya Mtoto wa Afrika
Mgeni rasmi akisamiana na wachezaji
Mgeni rasmi akisamiana na wachezaji
Timu ya wasichana Goronga sekondari VS Nyanungu Sekondari Picha ya pamoja
Timu ya Nyanungu Sekondari na Goronga Sekondari zilizoingia fainali katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi
Mchezo ukiendelea katika viwanja vya shule ya Msingi Masanga
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika viwanja vya shule ya Msingi Masanga Mwl Ryoba Mariba ambaye ni Afisa Taaluma kwa niaba ya Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini akiongea na watoto, wanachi na wakazi wa Masanga juu ya Madhala ya ukeketaji, Ndoa za Utotoni nakusisitiza suala zima la Elimu kwa watoto wate bila ubaguzi
Watoto wakisikiliza kwa makini
Zawadi kwa washindi katika michezo mbalimbali
Wachezji wa Timu ya wasichana Nyanungu Sekondari wakikabidhiwa seti ya Jenzi baada ya kuwabamiza Goronga Sekondari
Nyanungu Sekondari wakikabidhiwa zawadi seti moja ya Jenzi na kombe baada ya kulaza kichapo cha bao 3-0 Timu ya Goronga Sekondari katika Fainali hizo
Wakionesha Kombe Mabingwa
Picha za pamoja kwa wachezaji baada ya kukabidhiwa zawadi za jenzi hizo
Picha za pamoja kwa wachezaji baada ya kukabidhiwa zawadi za jenzi hizo
Picha za pamoja kwa wachezaji baada ya kukabidhiwa zawadi za jenzi hizo
PICHA ZOTE NA CLE0 24 NEWS
SIKIZA VIDEO HAPA CHINI