POLISI WAKAMATA MIRINGU, BANGI NA ZA NYARA ZA SERIKALI.




. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu,Kamishina Msaidizi wa Polisi Jonas Mahangaakiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) vipande viwili vya ngozi ya Twiga alivyokamatwa navyo Masuke Ndongo (40) na wenzake wawili katika hifadhi ya serengeti.



Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu,Kamishina Msaidizi wa Polisi Jonas Mahangaakiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo Pichani) kichwa cha nyumbu alichokamatwa nacho mtuhumiwa Masuke Ndongo (40) na wenzake wawili katika hifadhi ya serengeti wilayani Bariadi mkoani hapa.

Madawa ya kulevya aina ya mirungi baada ya kukamtwa yakiwa yamefungwa katika uzito tofauti yote yakiwa na uzito wa kilo 1000.




Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu,Kamishina Msaidizi wa Polisi Jonas Mahanga akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) baada ya kukamata madawa ya kulevya na nyara za serikali.


Gari aina ya Toyota Mark II T.300 DDW inayomilikiwa na Isabirye Addy mkazi wa Mwanza ikiwa katika kituo cha polisi Nyashimo baada ya kutelekezwa na Dereva Kaombwe Gaspal alipokuwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya Mirungi ikiwa imepakia kilo 1000.

Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.

JESHI la Polisi mkoani Simiyu limefanikiwa kukamata madawa ya kulevya aina ya Mirungi yenye uzito wa kilo 1000 zilizokuwa zikisafirishwa kwenye gari dogo kutokea Sirari kulekea jijini Mwanza kwa ajili ya Biashara.


Aidha Jeshi hilo pia limekamata nyara za serikali ndani ya hifadhi ya Serengeti ambapo mtuhumiwa alikamatwa akiwa na ngozi za swala, nyumbu,twiga, nyemela na kichwa cha nyumbu.

Akiongea na waandishi wa Habari, Kwa niaba ya kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu, Kamishina Msaidizi wa Polisi mkoani hapa Jonas Mahanga alisema kuwa mnamo tarehe 18/6/2017 katika kijiji cha yitwimila B, kata ya kiloleli wilayani Busega ilikamtwa gari aina Toyota Mark II lenye no T 300 DDW iliyokuwa imepakia magunia yenye uzito wa kilo 1000 ya madawa ya kulevya aina ya mirungi.

Kamanda Mahanga alisema kuwa dereva wa gari hilo aitwae Kaombwe Gaspal alifanikia kutoroka kabla hajakamatwa na askari baada ya kulitelekeza gari hilo na juhudi za kumtafuta dereva huyo zikiendelea.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo limefanikiwa kukamata nyara za serikali katika hifadhi ya Serengeti wilayani Bariadi mkoani hapa ambapo askari wakiwa katika msako walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa ujangili akiwa na ngozi za wanyamapori ambao swala, nyumbu, twiga na kichwa cha nyumbu na mikia yake.

‘’tumemkamata Masuke Ndongo (40) msukuma wa Damidami na wenzake wawili wakiwa na ngozi 01 ya swala, ngozi 03 ya nyumbu, ngozi ya nyemela, kichwa cha nyumbu, mikia 05 ya nyumbu na ngozi 02 za Twiga’’ alisema Kamanda Mahanga.

Aidha katika kijiji cha Msikula kata ya Lamadi wilayani Busega mnamo tarehe 11/06/2017 saa 3:00, askari wakiwa kwenye msako mkali walifanikiwa kumkamata Musa Kaniki (25), msukuma mkulima wa Lamadi akiwa na bhangi kilo 06 na amefikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria, aliongeza Kamanda Mahanga.

Aidha katika oposesheni mbalimbali jeshi hilo limefanikiwa kukusanya jumla ya Tsh 53,970,000/= na kati ya fedha hizo Shilingi 14,970,000/= zimetokana na makosa 499 ya madereva barabarani pamoja na waendesha pikipiki almaarufu kama bodaboda.

Jeshi la Polisi mkoani hapa limewataka wakazi wote wa mkoa huu kuachana na vitendo vya kihalifu na badala yake kujikita katika uzalishaji mali wa halali ili kuweza kukuza uchumi na pia wananchi walisaidie jeshi hilo kuwabaini wahalifu ili waweze kuchukuliwa hatua na kufikishwa katika vyombo husika za kisheria.


Powered by Blogger.