MWL: CHACHA HECHE ASAIDIA WATOTO WENYE MAHITAJI KIJIJI CHA KITENGA KATA YA BUMERA TARIME
Mwl Chacha Heche ambaye ni katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Mara akiwa katika picha ya pamoja baada ya kutoa msada wa Nguo, Viatu kwa watoto wa familia moja wenye mahitaji katika kijiji cha Kitenga kata ya Bumera Wilayani Tarime.
Watoto hao ni wa familia moja Baba yao ni Mgonjwa na wanaishi na Bibi yao ambaye ni mzee sana mwenye umri wa Miaka 81 na pia haoni hawajabaatika kwenda shule kwa sababu ya ugumu wa maisha na mwangalizi wa familia pia hawana mama mzazi hivyo suala hilio limemufanya Mwl Chacha Heche kuwatembelea wanafamilia hao kwa lengo la kuwapatia msaada wa nguo ili wafarijike kama binadamu wengine.
"Siku ya Jana nimetimiza nadhiri yangu ya kuhakikisha nawavisha watoto hawa wote wa familia moja wanaoishi na Bibi yao Mwenye miaka 81 mkazi wa kijiji cha Kitenga kata ya Bumera wilayani Tarime ambaye amepofuka macho,Nilimwomba Mungu anipe nguvu nirudi kwao, kwa Mara nyingine kuhakikisha nawavisha mavazi ili wasijione wapweke katika DUNIA" alisema Mwl Chacha Heche.
,Hata hivyo Chacha alisema kuwa utajiri sio Mali uliyo nayo katika bank Bali ulicho nacho moyoni,Dini ya Kweli ni ile inayohudumia wahitaji pia akatopa Shukurani kwa familia yake kwa kumpa moyo wa kuendelea kusaidia jamii kama kiongozi.
Na jukumu lingine la Viongozi pasipokujali itikadi za vyama wala dini ni kuendelea kusaidia watu wenye mahitaji wakiwemo walemavu, wagonjwa na watu maskini.
Mwl Chacha alipotembelea familia hiyo mara ya kwanza.
Kulia ni Bibi Nyaghin Mrimi81 ambaye anaishi na watoto hao pia haoni