Mwanaume Aoa Mwanaume Mwenzake bila Kujua Mtwara
Dunia imekwisha ndivyo unavyoweza kusema!! Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni...Kutoka Mkoani Mtwara tumepata habari kuwa mwanamme mmoja amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuoa mwanamme mwenzake bila kujua.
Hii imetokea katika Kijiji cha Mkahara, halmashauri ya mji wa Nanyamba, wilaya ya Mtwara, mkoani Mtwara ambapo mwanamme huyo amejikuta akivunja ukimya kuwa mtu aliyemuoa siyo mwanamke bali ni mwanamme kwani tangu amuoe hajawahi kupewa tendo la ndoa.
Inaelezwa kuwa jamaa huyo kaishi na mwanamme mwenzie kwa muda wa miezi minne na kila akitaka wafanye tendo la ndoa mwenzie hudai kuwa anaumwa na kwamba shughuli zote zinazofanywa na akina mama nyumbani ikiwemo kuosha vyombo,kujipodoa,kupika anafanya vizuri tu.