MULTICHOCE TANZANIA WAONYESHA MAPENZI, WAWAPA MSAADA WATOTO YATIMA




:Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo akikabidhi mashuka kwa Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madinnah kilichopo Tandale jijini Dar es Salaam Kuruthum Juma (wa pili kulia). Wa pili Kushoto ni Malkia wa taarabu Khadija Kopa na kulia ni Mwigizaji maarufu wa tamthilia ya Huba, Riyama Ali ambao ni mabalozi maalum wa DStv. Hafla hiyo ilifanyika jana katika kituo hicho ambapo vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mbili vikiwemo vyakula, mashuka, vyombo na mitungi ya kuzimia moto vilikabidhiwa

Kampuni ya Multichoice Tanzania imetoa zawadi ya sikukuu ya Idi kwa kituo chakulelea watoto yatima cha Al-Madinnah kilichopo Tandale jijini Dar es Salaam.Msaada huo wa vyakula na vifaa mbalimbali umekabidhiwa kwa kituo hicho naMeneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo katika hafla fupiiliyofanyika kituoni hapo ambayo pia ilihudhuriwa na mabalozi kadhaa wa DStvakiwemo malkia wa Taarab Khadija Kopa na muigizaji maarufu wa filamu na Tamhtilia ya HUBA , Riyama Alli.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Shelukindo amesema kwa takribanmiaka mitano mfululizo Multichoice imekuwa ikikisaidia kituo hicho kwa mambombalimbali.



Amesema wanafanya hivyo kwa kutambua kuwa malezi ya watotowaishio katika mazingira magumu ni jukumu la kila mtu na kila taasisi. “Tunatambuakuwa jukumu la kuwalea watoto kama hawa ambao kwa sababu moja ama nyinginewamejikuta katika mazingira magumu ni letu sote. Hawa ni ndugu zetu, watoto wetu,na pia ni tegemeo kubwa kwa taifa letu, hivyo kuwasaidia ni jukumu letu”

Amesema mbali na kwamba Multichoice imekuwa ikikisaidia kituo hicho mara kwamara kwa kuwapa vyakula na mahitaji mengine, lakini pia waliamua kufadhiliuanzishwaji wa mradi wa ushonaji ambao unakisaidia kituo hicho katika kujiingiziakipato. “Tunajua kuwa chakula, malazi na mambo mengineyo ni muhimu kwa maishaya kila siku ya vijana wetu, lakini pia tuliona ni busara kuwawekea kamradi japokadogo ambako wataweza kujipatia kipato. Tumefurahi sana kuona mradi huuunaendelea na tunaamini kuwa wataweza kuuendeleza na kuukuza ili uwasaidiaZaidi.” Alisema Shelukindo.

Kwa upande wake Mkuu wa kituo hicho Mama Kuruthum Juma ameishukuruMultichoice Tanzania kwa msaada wao wa mara kwa mara kwa miaka mingi sasa.


Amesema kitendo cha Multichoice Tanzania kukisaidia kitua hicho kwa mambombalimbali hususan mradi wa ushonaji kumewasaidia sana katika kujipatia kipatajapo kusaidia gharama za uendeshaji kituo hicho ambazo ni kubwa.

“Kwa kweligharama za uendeshaji kituo ni kubwa sana na kama mnavyofahamu watotowanaolelewa hapa hawana uwezo na wengi wao hawana wazazi, hivyo ni jukumuletu kuwalea, kuwapa matibabu, na pia kuwasomesha, hili kwa kweli ni jukumukubwa na tunahitaji msaada kutoka kwa wadau mbalimbali” alisema Mama Kuruthum

Amesema idadi ya watoto imekuwa ikiongezeka lakini kituo hakina uwezo mkubwakutokana na ufinyu wa eneo na bajeti hivyo akawaomba wadau wengine kuangaliauwezekano wa kukisaidia kituo hicho ili kiweze kuhudumia watoto wengi Zaidi.

Naye Malkia wa Taarabu – Khadija Kopa amesema amefarijika sana kuonaMultichoice Tanzania inawajali watoto hususan wale waishio katika mazingiramagumu ambao aghalabu husahaulika na jamii. “Kwakweli Multichoice Tanzania wamefanya jambo la maana sana. Ni vyema tukaunganisha nguvu zetu kuwaleahawa watoto wetu kwani nao wana haki kama watoto wengine” alisema Kopa.

Naye muigizaji Riyama Ali amepongeza jitihada zinazofanywa na MultichoiceTanzania pamoja na uongozi wa kituo cha Almadinna katika kuwasaidia watoto hao.

“Watoto hawa ni hazina ya taifa. Tukiwasaidia hawa wakakua vizuri, wakapata elimunzuri, kesho na keshokutwa tutapata wabunge humu, mawaziri, wakurugenzi,wanamichezo, wasanii na kadhalika. Tushirikiane kuwalea na hili ni jukumu letu sotena ni kitu kinacholeta Baraka” alisema Riyama.

Kituo cha Al-Madinnah Orphanage Centre kilianzishwa mwaka 2004 na kwa hivi sasakituo hicho kinahudumia jumla ya watoto 65 ambapo 40 kati yao ni wavulana na 25wasichana na wengi wao ni wanafunzi wa shule za msingi.
Powered by Blogger.