Video, Picha katika Matukio Dc Luoga azungumzia suala la kuvamiwa kwa Mgodi wa ACACIA Nyamongo.




Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorius Luoga akiongea na Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji na watendaji wa kata kuhusu suala zima la uvamizi wa Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu Nyamongo hii leo katika Ukumbi wa  Shule ya Sekondari Ingwe ambapo amewataka Wenyeviti wa Vijiji na watendaji kwa kushirikiana na Madiwani waendelee kuhubiri suala zima la amani huku serikali ikiendelea vyema na mazungumzo na Mwekezaji ili wale wote wanaodai fidia waweze kulipwa Fidia zao.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya huyo amekabidhiwa mapendekezo yaliyotolewa na Madiwani na wenyeviti kutoka vijiji vinavyozunguka mgodi wa ACACIA na kuhaidi kuyafanyia kazi.

Katika kikao hicho imebainika kuwa kuhusu suala zima la uvamizi wa Mgodi ambao ulifanyika hivi Karibuni watu wengi wanatoka Nje ya Wilaya  ya Tarime na Maenneo mengine tofauti na Nyamongo hivyo serikali imejipanga kwa lengo la kuendelea kudumisha Amani ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali wale wate wanaoshiriki kuchochea maandamano.


Diwani wa Viti maalumu CHADEMA Philomena Tontola akichangia hoja  katika kikao hicho ambpo alisema kuwa katika uvamizi huo akina mama wakiwemo wajawazito walishiriki jambo ambalo ni hatari kwao hivyo amelaani vikali kitendo hicho na kuomba serikali kusikiliza kilio cha Wanachi hao.


Diwani wa kata ya Kibasuka Royce Manyata akiongea katika kikao hicho ambaopo amesema kuwa yeye hayuko tayari kwenda kutetea Mwanachi yeyote atakayeshiriki katika uvamizi wa Mgodi bali wanchi wasubiri serikali ifanye kazi yake huku akiomba Mgodi kuendelea kudumisha suala zima la mahusiano mema na Wananchi

Diwqani wa kata ya Kemambo CCM Rashid Bugomba akiongea katika kikao hicho ambapo amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na serikali huku akipongeza kamati ya ulinzi na usalama wilaya kwa kumaliza vyema suala ambalo lilijitokeza la uvamizi wa Mgodi wa ACACIA

Mourice Okinda OCD Nyamwaga akizungumzia suala zima la uvamizi wa Mgodi huo ambapo amezidi kuwaomba wenyeviti wa vijiji kuendelea kuhasisha suala zima la Amani na kulaani kitendo cha akina mama na wajawazito kuingia ndani ya Mgodi ili kuchukua Mawe yenye dhahabu kitu ambacho ni hatara 


"Sisi jeshi la polisi tulikuwa tunatimiza wajibu wetu tulishindwa kupiga mabomu ya machozi sejemu yenye akina mama na watoto wengine wajawazito lakini mpaka sasa tunashikilia wati 66 na wengine tunaendelea kuwatafuta yule yeyote ambaye anashiriki kuchochea pjeshi la polisi tunaendelea na kazi zetu"alisema Okinda.


Mkurugezni wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Apoo Castro Tindwa akiongea na waandishi wa Habari ambapo amesema kuwa serikali itaendelea kufanya shughuli zake vyema kwani halmashauri inategemea mapato kutokana na shughuli za Mgodi huo hivyo mazungumzo yanaendelea ili wanachi wanaodai fidia waweze kulipwa na shughuli kuendelea na kulaani kitendo cha wanachi kuvamia Mgodi huo


                   Wenyeviti wa Serikali za Vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Acacia Nyamongo wakiwa katika Kikao cha pamoja ili kurejesha yale yaliyozungumzwawa katika vikao.
Powered by Blogger.