CRDB WATOA MSAADA KWA WALEMAVU WA NGOZI (ALBINO).



Afisa wa benki ya CRDB tawi la Bariadi Josephati Katoto akimkabidhi mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa Ngozi (albino) cha Bikra Maria Sister Hellena Ntambulwa mafuta kwa ajili ya kupikia pamoja na vitu mbalimbali vya vyakula katika kituo hicho


Meneja wa benki ya CRDB tawi la Bariadi Kishosha pamoja na Afisa wa benki hiyo Josephati Katoto akimkabidhi mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa Ngozi Sister Hellena Ntambulwa mafuta kwa ajili ya kupikia pamoja na vitu mbalimbali vya vyakula katika kituo hicho .


                             Na COSTANTINE MATHIAS, SIMIYU. 

Benki ya CRDB tawi la Bariadi mkoani Simiyu imetoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO) na yatima cha chenye Makao ya Bikra Maria kilichopo wilayani Busega mkoani humo.

Vyakula vilivyotolewa ni pamoja na mchele kilo 100,sukari kilo 25 mahindi kilo 100 pamoja na vinywaji mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia mahitaji ya chakula kwa watoto 65 wanaolelewa katika kituo hicho.

Akikabidhi msaada huo jana Afisa wa benki hiyo Josephati Katoto alisema kuwa msaada huo wenye thamani ya milioni 2 utawasaidia watoto kupunguza mahitaji ya chakula.

Katoto alisema jukumu la malenzi kwa watoto hao linapaswa kufanywa na watanzania wote pamoja na taasisi mbalimbali ili kupunguza wimbi la wananchi tegemezi hasa katika vituo vya kulelea.

“malezi ya watoto hawa ni jukumu letu sote kama watanzania kuhakikisha tunawasaidia ili waweze kupata elimu itakayowakomboa kimaisha na kupiga vita mauji ya watu hawa”alisema Katoto.

CRDB ilitembelea kituo hicho ikiwa ni mwendelezo wa kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika inayoadhimishwa duniani kote ambapo watumishi wa benki hiyo walipata wasaa wa kufurahia na watoto pamoja na kutoa vyakula na vinywaji.

Aidha katoto amezitaka taasisi na asasi za kiraia kujaribu kujitoa kwa moyo kundi hilo ambalo likipata makuzi mazuri litaweza kujiongoza lenyewe hapo baadae pasipo msaada hasa zaidi wakipata mazingira mazuri ya kupata elimu.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo hicho Sister Hellena Ntambulwa ameishukuru Benki hiyo na amezita benki zingine kuiga mfano kwa kutoa misaada katika vituo vya kulelea watoto wenye ualbino na yatika kwani kufanya hivyo kutawafanya watoto hao kuendelea kuwa na afya njema na kupata elimu bora.

Pia alisema kituo hicho kinawatoto 65 ambapo baadhi ya wazazi wamewatelekeza bila kwenda kuwaona wao hivyo inawanya waishi katika kituo hicho kama yatima ambao hawana wazazi.

Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wameiomba serikali kushirikiana na wadau mbalimbali kupeleka misaada ya chakula ambayo itawafanya watoto hao waendelee kuishi vizuri katika kituo hicho.






Powered by Blogger.