BMT WAAGIZA, WATAKAOSHINDA UCHAGUZI TFF KUACHIA NAFASI ZAO MKOA, WILAYA
Baraza la Michezo la Taifa la (BMT), limeagiza wagombea wa nafasi za uongozi TFF wazipitie kanuni za baraza la michezo.
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amesema kulikuwa na mkutano kati ya baraza na shirikisho na mambo kadhaa yameagizwa.
“Kanuni ya nane, kipengele cha kwanza na cha pili, inaangiza wagombea watakaoshinda nafasi wanazowania ndani ya TFF, watatakiwa kuachia nafasi yoyote ya mpira wa miguu wanayoshikilia katika mkoa au wilaya.
“Pia BMT imeagiza wanafamilia wa soka kuachana na tabia ya kushika nafasi mbili kwa wakati mmoja.
“Mwisho imesisitiza suala la kusisitiza kuwepo kwa haki, pia amani na kuepuka masuala yoyote ya uchochezi,” alisema Alfred.