Angalia Video: Wenyeviti wa Mitaa CHADEMA Halmashauri ya mji wa Tarime w...
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa akiongea na wenyeviti wa Mitaa katika Halmashauri ya Mji wa Tarime juu ya ukusanyaji wa kodi ya Majengo hii leo, ambapo kikao hicho hakikufikia mwisho baada ya wenyeviti wa Mitaa kupitia CHADEMA kususia kikao hicho
Wenyeviti hao wamesusia kikao hicho baada ya kuleta hoja ya ofisi ya mwenyekiti wa kata ya Nyamisangura kuwa jengo hilo ni mali ya CCM na kupakwa rangi ya Chama hii leo ndipo kulitokea hali ya kutoelewana baina ya wenyeviti hao na mkurugenzi na Mkurugenzi kuamua kutoka nje na kikao kuharibika.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa akiongea na wenyeviti wa Mitaa katika Halmashauri ya Mji wa Tarime juu ya ukusanyaji wa kodi ya Majengo
ANGALIA VIDEO CHINI ILIVYOKUWA KATIKA KIKAO HICHO