Angalia Video: Wenyeviti wa Mitaa CHADEMA Halmashauri ya mji wa Tarime w...


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa akiongea na wenyeviti wa Mitaa katika Halmashauri ya Mji wa Tarime juu ya ukusanyaji wa kodi ya Majengo hii leo, ambapo kikao hicho hakikufikia mwisho baada ya wenyeviti wa Mitaa kupitia CHADEMA kususia kikao hicho

Wenyeviti hao wamesusia kikao hicho baada ya kuleta hoja ya ofisi ya mwenyekiti wa kata ya Nyamisangura kuwa jengo hilo ni mali ya CCM na kupakwa rangi ya Chama hii leo ndipo kulitokea hali ya kutoelewana baina ya wenyeviti hao na mkurugenzi na Mkurugenzi kuamua kutoka nje na kikao kuharibika.



Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa akiongea na wenyeviti wa Mitaa katika Halmashauri ya Mji wa Tarime juu ya ukusanyaji wa kodi ya Majengo




Wenyeviti wa Mitaa , Watendaji wa kata na Mitaa katika kikao cha pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara.

Pamba Chacha ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Songambele Pia Mwenyekiti wa Wenyeviti CHADEMA Halmashauri ya Mji wa Tarime akifafanua jambo baada ya kikao hicho kuvurugika ambapo amesema hawako tayari kuendelea kukusanya kodi ya majenzo bali Halmashauri watumie watendaji wa Mitaa na kata.

 
ANGALIA VIDEO CHINI ILIVYOKUWA KATIKA KIKAO HICHO
Powered by Blogger.