ALLY MAYAY, MTEMI RAMADHANI KUCHUKUA FOMU KUWANIA URAIS TFF
MAYAY
Ally Mayay anatarajia kuchukua nafasi ya kuwania Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Taarifa zinaeleza Mayay ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, atachukua fomu hizo leo.
MTEMI
Wakati Mayay anachukua fomu, mshambulizi matata wa zamani wa Simba, Mtemi Ramadhani “Mangi” naye anatarajia kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Makamu Rais wa TFF.
Imeelezwa, wachezaji hao watasindikizwa na wanasoka wa zamani wa klabu mbalimbali za soka.