WATU WATANO WAFARIKI KWA KUANGUKIWA NA MTI ARUSHA



Watu watano wamefariki dunia katika kijiji cha Ngiresi wilaya ya Arumeru mkoani Arusha baada ya mti mkubwa kuangukia nyumba waliyokuwa wamelala usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa kuanguka kwa mti huo kumetokana na athari za mvua zinazoendela kunyesha.

Amesema kuwa waliofariki dunia ni watoto watatu ambao walikuwa wanafunzi na vijana wa wiwili. Kamanda huyo amesema taarifa zaidi atatoa hapo baadae.

Powered by Blogger.