Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba inaibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Dakika ya 92: SIimba wanapoteza muda kwa kupigiana pasi fupifupi.
Dakika ya 90: Mashabiki wa Simba wanashangilia wakiamini timu yao imeshapata ushindi.
Dakika ya 86: Simba wamepunguza kasi ya kushambulia.
Dakika ya 84: Lyon wanasogea kwenye lango la Simba mara kadhaa.
Dakika ya 80: Timu zote zinaendelea kucheza kwa kuw aan tahadhari kubwa.
Dakika ya 77: Thomas Morris wa Lyon anapata kadi ya njano, analalamika kuwa hakufanya kosa lakini mchezo unaendelea.
Dakika
ya 70: Kasi ya mchezo imepungua kiasi kutokana na mvua, benchi la
ufundi la Simba linaendelea kuonyesha kuwa na presha muda wote licha ya
kwa timu yao ndiyo ambayo inaongoza hadi sasa.
Dakika ya 65: Anatoka Mohamed Ibrahim 'Mo' wa Simba anaingia Juma Luizio.
Dakika ya 64: Lyon wanafanya mabadiliko, anaingia Abdallah Mgui anatoka Kibingu.
Dakika ya 62: Kichuya anashindwa kuendelea kucheza, anatolewa na nafasi yake inachukuliwa na Mwinyi Kazimoto.
Dakika ya 61: Kichuya anachezewa faulo, yupo chini anatibiwa.
Dakika
ya 58: Mchezo sasa umechangamka baada ya bao la pili la Simba,
inavyoonekana Simba wanataka kupata bapo la tatu huku Lyon nao
wakipambana kusawazisha.
Dakika
ya 56: Beki wa African Lyon, Hamad Waziri anajifunga katika harakati za
kuokoa hatari, ilipigwa krosi kutoka upande wa kulia mwa lango lao,
akataka kuupiga kwa nyuma, lakini mpira unaingia wavuni kwake.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 53: Mvua inaendelea kunyesha, wachezaji wanateleza. Ufundi wa kuuchezea mpira umepungua.
Dakika
ya 49: Simba wanashindwa kupata bao, Mavugo anapata nafasi akiwa peke
yake, anapiga mpira unaopanguliwa na kipa, inakuwa kona.
Dakika
ya 47: Beki wa Lyon anafanya makosa, Mohamed Ibrahim wa Simba anaunasa
mpira lakini shuti lake linakosa nguvu na kudakwa na kipa wa Lyon.
Mchezo umeanza, kipindi cha pili, kuna mvua imeanza kunyesha kwenye Uwanja wa Taifa.
Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili.
HALF TIME
Dakika
ya 49: Mwamuzi anapuliza kipenga kukamilisha kipindi cha kwanza, sasa
ni mapumziko. Mchezo ulikuwa mkali, Lyon waliamka baada ya kufungwa bao.
Dakika
ya 47: Omar Abdallah anaipatia Lyon bao la kusawazisha baada ya mpira
kumkuta karibu na lango la Simba na kuachia shuti kali.
GOOOOOOOOOOOO!
Dakika ya 46: Lyon wanafanya mabadiliko ya wachezaji, anatoka Baraka Jaffar ambaye ameumia, ameingia Hamad.
Dakika ya 45: Zinaongezwa dakika nne za nyongeza.
Dakika ya 44: Ajibu anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo mchezaji wa Lyon.
Dakika ya 42: Simba wanapata nafasi ya wazi lakini Ajibu anakuwa ameotea.
Dakika
ya 37: Simba wanapata bao la kwanza, Ibrahim Ajibu aipatia Simba bao la
kwanza, anapiga shuti kali kutoka nje ya eneo la 18, mpira unamgonga
kidogo beki wa Lyon na kujaa wavuni.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!
Dakika ya 34: Omary Salum wa African Lyon anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo Kichuya.
Dakika ya 30: Beki wa Simba, Boukungu anapanda mara kadhaa mbele kusaidia kutengeneza mashambulizi.
Dakika ya 28: Kichuya anawatoka walinzi wa Lyona na kupiga shuti kali lakini linatoka nje la lango.
Dakika ya 24: Simba wanaendelea kutawala mchezo.
Dakika ya 18: Lyon wanafika langoni mwa Simba na kupata kona mara mbili mfululizo lakini wanashindwa kuzitumia vizuri.
Dakika
ya 15: Simba wanalishambulia lango la Lyona lakini Ajibu anashindwa
kutumia nafasi anayopata baada ya kutengenezewa nafasi na Kichuya.
Dakika
ya 13: Simba wameanza kutawala mchezo, wanaumiliki muda mwingi, jua
nalo limeanza kutoka kwa kuwa mvua imekuwa ikinyesha kwa wingi jijini
Dar.
Dakika ya 10: mchezo bado haujawa na kasi, timu zote ni kama zinasomana.
Dakika ya 5: Simba nao wanajibu mapigo kwa kushambulia kupitia kwa Laudit Mavugo.
Dakika ya 3: African Lyon wanafanya shambulizi kwenye lango la Simba.
Dakika ya kwanza mchezo umeanza.
Kikosi cha simba kinachoanza dhidi ya African Lyon hii leo