SHAKA AKAGUA MRADI MKUBWA WA MAJI KWA WANAFUNZI NA KUTOA VIFAA VYA UJENZI WA MIRADI MBALI MBALI YA KIMAENDELEO KWA MADIWANI WA KATA 15 JIMBO LA CHALINZE.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akizugumza katika Mkutano wa
ndani na Viongozi wa mashina ,tawi ,kata,wenyeviti wa vijiji na kata
pamoja na madiwani wa kata 35 jimbo la Chalinze
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze akitolea ufafanuzi juu ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze akitolea ufafanuzi juu ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020
Wananchi pamoja na Viongozi Wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa Tatu Toka kulia
akimkabidhi Vifaa Vya Ujenzi Mwenyekiti wa Halmashauri ndg: Said zikatim
kwa niaba ya madiwani wa kata 15 wa jimbo la Chalinze ambavyo ni Cement
pakiti 2,287 zenye thamani ya 22,013,500/= mabati 633 yenye thamani ya
TSH.14,559,00/=fedha taslim 5650000/= na fedha kwa ajili ya usafirishaji
kwa maeneo yote 3800,000/= vilivyo tolewa na mbunge wa jimbo la chalize
Mhe Ridhwani J Kikwete ikiwa ni ukamilishaji wa miradi ya maendeleo
yawananchi iliyoanzishwa katika kata 15 Jimbo la Chalinze
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa nne toka kushoto juu ya
jengo pamoja na viongozi mbali mbali wa chama na Serikali akikagua
Ujenzi Tank la maji Shule ya Moreto katika mradi wa maji kwa wanafuzi
wa shule hiyo uliogharimu jumla ya Sh milion Hamsini.
Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akifungua bomba la Maji yanayotoka
katika mradi wa maji Tank la Shule ya Moreto uliogharimu jumla ya
Shilingi milion Hamsini
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akiwatwika Ndo za Maji
kichwani Wanafunzi wa Shule ya Moreto Ilioko kata ya Lugoba Jimbo la
Chalinze.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondali Moreto wakiwa wamebebelea ndoo za maji
PICHA NA FAHADI SIRAJI