SABABU 10 KWANINI USICHUNGULIE NA KUPEKUA SIMU YA MPENZI WAKO

1. Kuna mwanaume ambaye kila siku anamtongoza na alishamkataa mara nyingi lakini jamaa hakati tamaa, kila siku anatuma meseji za ajabu ajabu na mkeo anazifuta. Siku ukiziona utadhani anakusaliti na hutamuamini tena na huo ndiyo utakuwa mwanzo wa ugomvi wenu.


2. Kuna mwanamke pale ofisini, jirani yenu au mtaani tu anamtaka na anashindwa kumuambia au ameshamuambia na mumeo hana habari naye, lakini yule dada haishi kutuma sms hata za salamu tu, namaneno kama “missing u, uko poa D, lunch leo juu yangu, upo dear, Mbona leo hujaniaga…” Ukiona utashtuka na hutamuelewa hasa kama unamfahamu huyo mwanamke.

3. Kuna rafiki yake ambaye wanachat ujinga wa mambo ya mapenzi na kutaniana mara kwa mara ukiuona huo ujinga na namna wanavyotaniana unaweza kudhani ni wapenzi na utaumia sana. Hata akikuambia hamna kitu hutaamini hata kama na wewe una rafiki wa namna hiyo.

4. Kuna group lao la Whatsapp la watu wa jinsia moja ambalo wanaongea kila kitu na moja ya vitu wanavypozungumzia ni mapungufu ya wapenzi wao ukiwemo wewe. Inawezekana wanaongea kwajaili ya kufurahishana tu au kujaribu kusaidiana kuyabadilisha na kukabiliana nayo lakini utakapoona utaumia na inaweza kuwa sababau ya kutokujiamini na kuhisi anakusaliti.

5. Ana yule X wake mmoja ambaye mpaka sasa haamini kuwa kaachwa na bado anatuma sms hata akibadili namba yeye yupo tu. Mara kadhaa hukumbushia namna walivyokuwa pamoja, ukiona meseji zake utahisi kuwa labda wamerudiana kimya kimya kupasha kiporo, utaumia bure.

6. Kuna mambo anafanya kimya kimya na ndugu zake ambayo ni ya kawaida hata wewe unafanya na ndugu zako lakini hujamshirikisha ila ukiona utaanza kuwaza kuwa anawapenda ndugu zake kuliko wewe. Meseji moja tu inaweza kuondoa imani kwa mwenza wako na kuleta ufa kwenye ndoa yako.

7. Kuna kitu alifanya bila kukuambia na alikuwa aanachat na rafiki yake hicho kitu hivyo ukiona utahisi kuna mengine mengi ambayo hakuambii. Umaminifu utapotea na wewe unaweza kuanza kufanya mambo yako kimya kimya na huo ndiyo mwanzo wa kuchukiana na kutengana.

8. Nikuvunja uaminifu, kwamba unapoanza kumchunguza inamaana humuamini na hii si mbaya kwake bali kwako kwani hata usipokuta kitu utaanza kuwaza labda kafuta na ukikuta utaumia zaidi kwa maana hiyo haikusaidii chochote unajiumiza mwenyewe.

9. Unatafuta tu maumivu ambayo huna hata haja ya kuyapata. Ukishagundua ukamuambia akakana au akakubali akakuomba msamaha utafaidika nini? Kukuomba msamaha si kwamba ataacha ataendelea kufanya lakini sasa tofauti nikua utakuwa ukijua kuwa anafanya na ukimuona yule mtu anayefanya naye ni maumivu tu, sasa kwanini ujitese.

10. Kuchungulia simu ya mwenza wako haisaidii chochote, wasaliti wengi huwa makini hufuta meseji za mapenzi na wengine wana mpaka namba kwaajili ya michepuko. Meseji nyingi zinazofumaniwa huwa ni za bahati mbaya na wakati mwingine si za michepuko bali ni marafiki tu wa kawaida. Mwisho bado na sisistiza kama huna mpango wa kumuacha usimchunguze.

Powered by Blogger.