Kikosi
cha Hull City kimeporomoka kutoka Ligi Kuu England. Lakini wadhamini
wake, kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa, imeendelea kubaki
kwenye Ligi Kuu England.
SportPesa wataendelea kubaki kwenye Ligi Kuu England baada ya kutangaza udhamini na Everton, moja ya timu kubwa za ligi hiyo.
Udhamini
huo ulitangazwa jana na kuifanya SportPesa kuwa wadhamini wapya
watakaoonekana kwenye vifua vya wachezaji na mashabiki wa Everton
kuanzia msimu ujao kwa kuwa mkataba huo unaanza Juni Mosi, mwaka huu.
Kwa hapa Tanzania, tayari SportPesa ni wadhamini wa Simba SC.