MKUU WA MKOA WA MWANZA AHITIMISHA MAADHIMISHO SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI, KITAIFA JIJINI MWANZA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amehitimisha kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliyofanyika kitaifa Jijini Mwanza, Mei 02 na 03,2017 .
Mongella amewasisitizia wanahabari kujikita zaidi katika weledi kwenye utendaji wao wa kazi ili kuondokana na migogoro inayoweza kujitokeza wakati wakitimiza majukumu yao.
Amewahimiza zaidi waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi na utafiti wa kina katika habazi zao huku akihimiza zaidi ushirikiano.
#BMGHabari
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed
Msangi (kushoto) akifuatilia maadhimisho hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania,
Salome Kitomari.
Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa
Habari nchini UTPC, Deogratius Sonkolo (kulia) na Mwenyekiti wa Jukwaa
la Wahariri nchini TEF, Theophil Makunga (kushoto), wakifuatilia
maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa
Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Abubakar Karsan,
akichangia mada kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Duniani, kitaifa Jijini Mwanza