Mkuu wa mkoa wa mara Dkt. CHARLES mlingwa amemuagiza Mkurugenzi huyo kufanya mabadiliko ya wakuu wa idara katika kitengo cha hazina na Mipango katika idara hizo kwa kuwa havina ufanisi wa utendaji wao wa kazi unaopelekea kuchelewesha kwa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.
Mvutano uliokuwepo wa mgawanyo wa asilimia ya Mgodi wa Cata Mining ulioko katika halmashauri ya Wilaya ya Musoma zimekwisha baada ya kuwepo kwa makubaliano ya kugawana mrahaba huo ulioko Kijiji cha Kataryo huku baadhi ya madiwani wakiiomba serikali ya Mkoa kuangalia upya suala hilo kwani mipaka yake iko halmashauri ya Musoma na si Butiama.
Akizungumza katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani katika halmashauri ya Musoma,Mkuu wa Mkoa wa Mara. Dk.Charles Mligwa alisema kuwa kutokana na mzozo uliokuwepo wa mrahaba uende wapi, halmashauri hizo zimekubaliana kugawana sawa kwa sawa kwa asilimia 50.
‘’Niliwashangaa kwa nini mnazozana na huku nchi hii ni yetu wote,mnakuwa kimusoma musoma,nani anastahili kupata mrahaba, hivyo mlivyofanya ndo uzalendo, angalie Mara kwanza…angalia Mkoa wa Mara,hivyo halmashauri itaongeza lengo la makusanyo kutokana na mrahaba ambao utaanza kuwekwa kesho baada ya nyie kukubaliana’’ Alisema Mligwa.
Alisema kuwa hazima ya serikali ni kuona halmashauri zinakuwa na uwezo wake zenyewe kwa kuwa na makusanyo yanayozidi lengo ambapo pia amewapongeza watendaji wa halmashauri hiyo kuvuka lengo la makusanyo na kukusanya asilimia 81.
Aliongeza kuwa kwa kuwa tayari halmashauri imekubali kugawana mrahaba wa mgodi huo makusanyo yataongezeka na kuwa zaidi ya asilimi 100.
Aidha amezipongeza halmashauri hiyo kupambana na uvuvi haramu ambao umeongeza mapato na kuwataka kutokomeza uvuvi haramu ambao unaua mazalia ya samaki na watendaji kuendelea kupambana na uvuvi haramu.
Aliongeza’’Uvuvi haramu umesababisha kuua viwanda vya samaki kutokana na viwanda kufugwa ambapo Manispaa ya Musoma ilikuwa na viwanda vipatavyo vinne lakini mpaka sasa vinavyofanya kazi kimebaki kimoja, hivyo unaweza kuona ni jinsi gani wananchi wameathirika kwa kukosa ajira na sera ya Rais ya kuwa na viwanda ipo, hivyo watendaji wanapaswa kuhakikisha uvuvi haramu unatoweka’’.
Amewataka pia kuepukana na matumizi yasiyo ya lazima na kuwataka kikao kijacho cha baraza la madiwani cha mwezi wa saba kufanyika katika kata ya Murangi na kumtaka Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Frola Yongola kufanya maandalizi mapema ili aandae baraza hilo kupunguza gharama.
Pia amemuagiza Mkurugenzi huyo kufanya mabadiliko ya wakuu wa idara katika kitengo cha hazina na Mipango katika idara hizo kwa kuwa havina ufanisi wa utendaji wao wa kazi unaopelekea kuchelewesha kwa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.
‘’Sina nia mbaya ya kumuadhibu mtumishi kama anafanya vizuri kazi yake bali ni kuhakikisha rasilimali watu vizuri ili kuweza kukua kama kuna mtu hana sifa aondolewe''Alikazia.Mlingwa
Naye diwani wa kata ya Buringa, Mambo Japan alisema kuwa pamoja na makubaliano hayo mgodi huo uko katika kata ya kataryo na wakati wanagwa kuna ramani zinazoonyesha kuwa eneo hili ni Musoma huku wakishirikiana na maafisa ardhi wallikwenda kubadilisha ramani hivyo ameiomba serikali kujua mgodi uko wapi ili mrahaba uende sehemu huska.
‘’sisi tuko hapa kwa niaba ya wananchi, kutaka halmashauri iende tunaomba mkurugenzi kuweka utaratibu kati ya madiwani na watendaji wa halmashauri na kwa upande wa uvuvi haramu mabwana samaki wapo wana makokoro zaidi ya 10 na wamewafumbia macho, endapo serikali haitachukua hatua uvuvi haramu hautaisha’’Alisema Japan.
Naye Diwani wa kata ya Suguti Dennis Ekwabi aliiomba serikali kuangalia endapo kuna uwezekanao wa kuwapatia chakula wananchi walioathirika na njaa kutokana na wadudu waharibifu wanaoharibu mahindi ambalo ni zao kubwa la chakula na biashara katika Wilaya hiyo na Mkoa wa ujumla.
Akijibu hoja zao Mkuu wa Mkoa alisema haiwezekani viongozi wakawa hawana ushirikiano kati ya watendaji wa halmashauri na madiwani na endapo maafisa ardhi wapo katika mtandao wa uvuvi haramu waondolewe kazini na endapo kuna uhakika na wanaojihusisha na wako katika mtandao wa wavuvi haramu waondolewe na wapelekwe sehemu nyingine
|