MCHUNGAJI WA KANISA AKAMATWA KWA KUOA MKE WA MUUMINI WAKE AKIDAI KAOTESHWA NA MUNGU
Mchungaji
wa kanisa la huduma katika roho wilayani Karagwe mkoani Kagera Jafece
Josephat anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo baada ya kumuoa
mke wa muumini wake na kuanza kuishi naye kama mke na mume akidai
ameoteshwa na Mungu.
Mchungaji huyo amekamatwa jana baada ya kamati ya ulinzi na usalama na kamati ya amani na maadili ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Godfrey Mheruka kufika kanisani hapo na kupata ukweli juu ya jambo hilo baada ya pande zote akiwemo mchungaji wa kanisa Josephat, mwanamke aliyefahamika kwa jina la Domina Damian na mme wake wa mwanzo Donath Appolo kueleza ukweli jinsi walivyooteshwa mpaka hatua ya mke kuolewa.
Mkuu wa Wilaya Akimhoji Mchungaji
Mkuu wa Wilaya akimhoji mume wa huyo mwanamke