LOWASSA ALAANI SERIKALI KUZUIA KONGAMANO LA DEMOKRASIA DAR
Mjumbe
wa kamati kuu ya Chadema na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. Edward Lowassa
amelaani vikali kitendo cha serikali ya Mkoa wa Dar es salam kuzuia
kongamano la demokrasia lililopangwa kufanyika siku ya jana may 13,
Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Mhe.
Lowassa jana akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mikocheni, Dar
alisema kuwa amesikitishwa sana na serikali kuzuia kongamano ambalo
lilikuwa na nia njema ya kuzungumza kuhusu demokrasia na kujifunza
kutoka kwa watu mbali mbali jinsi ya kufanya siasa bila kukosea na
kurekebishana penye makosa.
Mjumbe
huyo aliendelea kufafanua kwamba hakuna tatizo kwa vyama vya siasa
kutofautiana mawazo kwani ndiyo demokrasia na ndiyo sababu kubwa ya
waandaji kushirikisha watu wenye taaluma tofauti tofauti katika
kongamano hilo.
"Chadema
kwa ujumla tunalaani sana kitendo cha Serikali ya Dar es salaam kuzuia
mkutano wa amani wa kuwaunganisha watanzania pamoja kwa kutumia
kongamano la demokrasia.
"Kitendo
ambacho kimefanywa ni kuminya demokrasia. Nia ilikuwa njema na ndio
maana waandaji wa kongamano waliweka picha yangu na kinana tukiwa
tunatabasamu hivyo hakuna dhambi kwenye kutofautiana mawazo"- alisema Lowassa.
Taarifa iliyotolewa jana kuhusu kongamano.
Hata
hivyo Mhe. Lowassa amekitaka chama cha Mapinduzi kutonyayasa upinzani
kwa kuwa hawataweza kukaa madarakani muda wote huku akiwatahadharisha
wakumbuke vyama vya ukombozi wa Afrika vilivyobaki madarakani ni ANC na
CCM.