Hata hivyo, makundi yote matatu yamejitokeza na kuwasilisha rufaa na
malalamiko yao Necta. Akizungumzia sakata hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki,
alisema jana bado kazi ya kushughulikia rufaa za waliokata kuhusishwa
na vyeti feki inaendelea na ikikamilika, umma utapewa mrejesho.