Na Saleh Ally
WAKATI
Ligi Kuu Bara inakwenda ukingoni, mbio za wafungaji zinaonekana
kuongozwa na wazawa ambao miaka mingi wanaonekana wamekuwa
wasindikizaji.
Kuna
baadhi ambao wamekuwa wakionyesha kujitutumua na wameendelea kuwa
katika vita hiyo mfululizo bila ya kuchoka hata kama hawatakuwa
wafungaji bora.
Angalau
John Bocco wa Azam FC amekuwa akionyesha njia. Lakini hivi karibuni,
ameonekana kupoteza mwelekeo katika ufungaji na huenda ile ishu ya
kuandamwa na majeraha mfululizo imempoteza.
Simon
Msuva anayecheza Yanga ndiyo yuko kwenye kizazi cha kukimbizana katika
kuwania ufungaji bora. Msimu mmoja uliopita, alikuwa mfungaji bora na
amekuwa akichuana vikali na Mrundi Amissi Tambwe ambaye ndani ya misimu
minne ndiye anaonekana ni mshambulizi bora kabisa hasa unapozungumzia
suala la kufunga mabao.
Ligi ya msimu huu ina radha nyingi sana na moja ambayo inavutia zaidi ni wale wanaochuana kuwania ufungaji bora.
Kwanza
hauwezi kusema nani ataibuka mshindi hasa unamuona mshambulizi kama
Tambwe anarejea katika kiwango chake mwishoni mwa ligi na sasa
amefikisha mabao 10.
Tambwe
ana uwezo wa kufunga hata mabao matano ndani ya mechi nne zilizobaki.
Lakini bado unaona Tambwe na Obrey Chirwa raia wa Zambia, wamezungukwa
na vijana wa Kitanzania wanaoonyesha pia wana uwezo mkubwa wa kucheka na
nyavu.
Anayeongoza
ni Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting akiwa na mabao 12 sawa na Msuva
ambaye pia amekuwa akipambana kuibuka kuwa kinara.
Walio
na mabao 11 ni Shiza Kichuya wa Simba na Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar
ambayo imeonekana inapigania kupata nafasi ya tatu ikichuana na Azam FC.
Bocco
hayupo mbali kwa kuwa ana mabao tisa baada ya kuwa amerejea na
anaonyesha ana kiwango kizuri. Kama atatulia uwezo wa kufikisha mabao 12
anao.
Chirwa
na Tambwe wamezungukwa na vijana wa Kitanzania na utaona si wale
wanaotokea Yanga na Simba tu, wako kutoka katika timu mbalimbali na
utaona zipo zile ambazo hata haziwanii ubingwa wa Bara.
Mfano
Abdulrahman, timu yake inapambana kujiokoa ili isiteremke daraja.
Lakini yeye ndiye anaongoza kwa ufungaji wa mabao, hili ni jambo zuri na
vizuri kama atatupiwa macho kwa ajili ya kuendelezwa zaidi.
Hali
kadhalika Mbaraka, naye timu yake haigombei kutwaa ubingwa. Lakini
anapambana kuwa mfungaji bora na anaochuana nao wote ukiachana
Abdulrahman na Bocco, waliobaki ni wale ambao timu zao zinazowania
ubingwa.
Awali,
ukiangalia listi ya wafungaji wanaowania ufungaji bora kwa asilimia 90,
wanakuwa wanatokea Simba au Yanga na kama ikiteleza kidogo basi ni
mchezaji kutoka Azam FC.
Mchezaji
anayeweza kufunga mabao 10 akiwa Yanga. Hakika hawezi kuwa na nafasi
nzuri ya ubora kama yule aliye Ruvu Shooting kwa maana ya viwango vya
wachezaji ambao wangeweza kumsaidia.
Angalia
Tambwe au Msuva wanaofunga mabao wakiwa wamezungukwa na nafasi nyingi
zaidi za kuweza kufunga. Viungo kama Haruna Niyonzima na Thabani
Kamusoko kwa Yanga au James Kotei na Said Ndemla na wengineo Simba.
Angalia
mabeki, Juma Abdul, Hassan Kessy au Mwinyi Haji kwa Yanga au Besala
Bokungu na Mohamed Zimbwe kwa Simba. Ni wachezaji wenye uwezo mkubwa wa
kutengeneza nafasi za ufungaji.
Kwa
wale walio Kagera au Ruvu Shooting wanaweza kuwa na wachezaji bora
lakini wanaokosa uzoefu au ubunifu wa juu kama wale walio Simba na Yanga
ambao wanaongezewa ujuzi na makocha wa kigeni au wazoefu pia wakipewa
hamasa ya juu na uongozi.
Kwa
wachezaji ambao wanaonyesha njia, vizuri wakatupiwa macho ya hamasa
ikiwezekana kuendelezwa zaidi kwa kuwa wanachoonyesha nyuma ya pazia
kwamba ni wazi wanataka kushikwa mkono ili wafanye zaidi ya hapo.