YANGA KAZI KWENU, COUTINHO ANASUBIRI SIMU YENU TU...
Kiungo
mshambuliaji wa zamani wa Yanga Mbrazili, Andrey Coutihno ambaye hivi
sasa anachezea Nongbua Pitchaya FC ya Thailand, amesema bado ana ndoto
za kurejea Jangwani.
Mbrazili
huyo aliondoka Yanga kwenye msimu wa 2014/2015 baada ya kusitishiwa
mkataba wake kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Mniger, Issofou
Boubacar aliyeichezea timu hiyo kwa miezi sita.
Coutihno kabla ya kutua kuichezea Nongbua Pitchaya alikuwa akicheza soka la kulipwa huko Myanmar barani Asia.
Akizungumza,
Coutinho amesema bado ana mapenzi ya klabu yake hiyo ya zamani
aliyoichezea kwa mafanikio ya kutwaa taji la ubingwa wa ligi kuu na Ngao
ya Jamii, mwaka 2014.
Coutihno
alisema angependa kurejea kuichezea Yanga mara baada ya mkataba wake
kumalizika lakini siyo hivi sasa huku akiwataja viungo wawili
Mnyarwanda, Haruna Niyonzima na Mzimbabwe, Thabani Kamusoko ambao
anatamani siku moja acheze nao.
"Nashukuru
hivi sasa ninaendelea vizuri na nimeondoka Myanmar nilipokuwa nacheza
soka na kuhamia nchini Thailand kwenye Klabu ya Nongbua Pitchaya FC.
"Bado
nina mipango ya kurejea kuichezea tena kwa mara ya pili Yanga kama
wakinihitaji nitarejea hapo baadaye mkataba wangu ukiwa umemalizika.
"Ninafurahi
maslahi ya huku Thailand ninayoyapata zaidi ya huko nilipokuwa nacheza
awali," alisema Coutihno anayetumia mguu wa kushoto.