WAZIRI UMMY ASISITIZA USAWA WA KIJINSIA KATIKA ELIMU.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiteta jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Rwekaza Mukandala (kulia) mara baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) alipomwakilisha Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anganisya.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam(DUCE) leo Jijini Dar es Salaam. Waziri Ummy alimwakilisha Makamu wa Rais katika ufunguzi wa Kongamano hilo.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Rwekaza Mukandala akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anganisya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) leo Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiteta jambo na  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Profesa Rwekaza Mukandala wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam(DUCE) leo Jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam(DUCE) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(hayupo pichani) alipomwakilisha Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu leo Jijini Dar es Salaam.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Rwekaza Mukandala akiteta jambo na Profesa Penina Mrama walipokutana katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) leo Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawasilisha mada katika Kongamano la Kimataifa kuhusu usawa wa kijinsia mara baada ya ufunguzi wa kongamano hilo leo Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wawasilisha mada katika Kongamano la Kimataifa kuhusu usawa wa kijinsia pamoja na baadhi ya waandaji wa kongamano hilo mara baada ya ufunguzi wa kongamano hilo leo Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).

Picha zote na: Frank Shija
 
Na Husna Saidi
Wazazi na walezi wametakiwa kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto wakike kutokana na Serikali kutoa fursa ya elimu bure kwa shule za Msingi na Sekondari ili kuongeza usawa wa kijinsia katika elimu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akifungua Kongomano la kwanza la Kimataifa la Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) ambapo alimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Jijini Dar es Saalam.
Waziri Ummy alisema kuwa uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano kutoa elimu bure  unatoa fursa zaidi kwa mtoto wa kike kunufaika na elimu tofauti na awali ambapo kutokana na hali ya maisha kuwa duni familia nyingi  zilitoa kipaumbele kwa mtoto wa kiume na kuwaacha wakike kufanya shughuli za nyumbani.
“Niwaombe wataalam wetu tuungane kwa pamoja kuhakikisha watoto wa kike wanapewa fursa sawa katika kujiunga na masomo, ata waliopata mimba kwa bahati mbaya wapewe fursa ya kurudi mashuleni,” alisema Waziri Ummy.
Aidha aliongeza kuwa ili kuleta asilimia hamsini kwa hamsini kwa wote wazazi wanatakiwa kuwahamasisha watoto wakike kupenda masomo ya Sayansi kwani inaonesha watoto wengi wakike hawana hamasa na masomo hayo.
Aidha aliupongeza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kuweza kufanikisha kuwa na wanafunzi wakike asilimia 38 wakati Serikali imefanikisha asilimia 32 ya wanafunzi wakike katika elimu ya juu.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala alisema kuwa tangia mwaka 1993 kulikuwa na mikakati ya kuwaweka watoto wa kike katika fani mbalimbali na kuwapa ujuzi ambapo imeonesha watoto wengi wa kike walikuwa wanaongoza kwa kufanya vizuri zaidi.
Nae Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anganisya alisema kuwa Kongamano hilo litaonesha nafasi ya mwanamke katika jamii na kuwa chachu kwa watoto wakike kupenda masomo ya Sayansi.
Serikali imejipanga kuja na mikakati mipya madhubuti ya kuboresha idadi ya wanafunzi wa kike hasa katika elimu ya juu ili kuleta usawa wa kijinsia.
 
Powered by Blogger.