SI UNAJUA TAMBWE AMEPOTEZA MAKALI YA KUFUNGA? MWAMBUSI HUYU HAPA ANAFAFANUA


Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, amefunguka kuwa, straika wake, Mrundi, Amissi Tambwe bado hajawa fiti licha ya kuanza kucheza mechi kadhaa tangu aliporejea akitokea kwenye majeruhi.

Tambwe ambaye alikuwa akisumbuliwa na jeraha la enka, wikiendi iliyopita alirejea uwanjani kucheza dhidi ya Prisons katika mchezo wa Kombe la FA na kufunga bao moja kwenye ushindi walioupata wa mabao 3-0.


Mwambusi amesema licha ya Tambwe kufunga bao katika mchezo huo, lakini bado hajawa fiti kwa asilimia zote kutokana na kukosa baadhi ya vitu vya kiufundi.


“Tambwe bado hajawa vizuri kwa asilimia zote licha ya kufunga bao muhimu kwa timu kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua hapo kabla.


“Lakini taratibu atakuwa fiti na kuisaidia timu kwenye michezo iliyosalia katika michuano tunayoshiriki ambayo yote tunataka kuchukua mataji yake,” alisema
Powered by Blogger.