SHUJAA SIMBU ALIVYOREJEA NA MAPOKEZI YAKE KUONGOZWA NA SERIKALI NA WADHAMINI WAKE MULTICHOICE TANZANIA


Balozi maalum wa DStv na Mwanariadha pekee wa Tanzania liyeshiriki mashindano ya London Marathon Alphonce Simbu amerejea nyumbani na kutoa onyo kali kwa wale atakaokabiliana nao kwenye mashindano yajayo ya dunia  yatakayofanyika mwezi Agosti jijini London.



Simbu ambaye alishika nafasi ya tano katika mashindano hayo na kujishindia kitita cha dola za marekani 10,000 aliwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na kulakiwa na maafisa mbalimbali akiwemo Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana, Meneja wa mwanariadha huyo Francis John 



Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Arusha muda mfupi baada ya yeye kuwasili Simbu aliwashukuru sana watanzania wote kwa moyo wao na jinsi walivyomuunga mkono na kumtakia kila la heri katika mashindano hayo. Amesema alifarijika sana na pia kupata moyo zaidi alipokuwa akipokea salamu kutoka kwa watanzania kote ndani nan je ya nchi.

Akizungumzia mashindano hayo, Simbu amesema yalikuwa na changamoto kama yalivyo mashindano mengine makubwa ya kimataifa kwani yalishirikisha vigogo ambao wengi wao wana uzoefu mkubwa katika mashindano mbalimbali na wengine pia ni washindi wa mashindano ya hapo awali.


Powered by Blogger.