SERIKALI YALIPA MADENI YA WALIMU TANZANIA
Serikali kupitia
Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imelipa madeni ya fedha za likizo
kwa walimu 86,234 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/17.
Hayo yamebainishwa
na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Stella Manyanya
wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.
“Serikali
inaendelea kulipa madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha za likizo
kwa walimu/Watumishi katika sekta ya Elimu”,Aliongeza Mhe.Manyanya.
Amesema kuwa
katika kipidi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi mwezi Juni, 2016 jumla ya
shilingi bilioni 22,629,352,309 zililipwa kwa walimu 63814, na pia
katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 hadi kufikia mwezi Machi, 2017
jumla ya shilingi bilioni 10,505,160,275 zimelipwa kwa walimu 22420.
Aidha katika
malipo haya jumla ya shilingi 13,415,410 zimelipwa kwa ajili ya madeni
ya fedha za likizo kwa watumishi wa chuo cha ualimu Korogwe.Akizungumzia
upande wa upandishaji madaraja Mhe.Manyanya amesema kuwakwa sasa
uhakiki wa watumishi unaendela na ukikamilika watapandisha madaraja kama
inavyotakiwa.
Aidha amesisitiza
kuwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imekuwa ikiwapandisha vyeo
watumishi wake wenye sifa kila mwaka ambapo katika mwaka 2015/16 Wizara
iliwapandisha vyeo watumishi 2272 kati yao watumishi 71 ni wa chuo cha
ualimu korogwe.
Uhakiki wa madeni
ya miaka ya nyuma unaendelea kuratibiwa na mamlaka husika na taratibu za
malipo zitakamilishwa kwa wale wanaostahili.
Na Daudi Manongi-MAELEZO.