|
Kundi la
vijana Wilayani Tarime Mkoani Mara wamepaza sauti ya pamoja kwa lengo la
kutetea Mwanamke pamoja na Mtoto wa kike kuwa nao wanahaki ya kumiliki Ardhi, Mali,
kushiriki katika mikutano na kufanya
maamuzi na siyo kila kitu kinafanywa na Wanaume jambo ambalo linazidi kupelekea Mfumo dume.
Wakichangia
mawazo kupitia Mdahalo ambao umeandaliwa
na shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto( CDF) chini ya Ufadhili wa Foundation for
Civil Society mdahalo huo umefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Kata Turwa Mjini
Tarime mkoani Mara kwa kushirikisha vijana 30 kutoka Mitaa yote ya kata ya Tuwa.
Sophia Temba
ni Afisa ulinzi na usalama wa watoto
kutoka shirika la CDF amesema kuwa Shirika hilo lime lenga kuwafikia vijana 150
huku akieleza lengo la Mdahalo huo ni kusikiliza maoni ya wanaume kuhusu
ushirikishwaji wa mwanamke katika jamii ya Kikurya ikiwa ni pamoja na
kuwajengea uwezo juu ya kupiga vita suala zima la ukeketaji.
Aidha Vijana
hao wameweza kutoa Maoni ya nini kifanyike kwa lengo la kunusuru watoto wa kike
ambao wanakumbana na suala zima la ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji na
Ndoa za utotoni ambapo wamesisitiza suala zima la elimu kuendelea kutolewa
katika jamii huska ili kutokomeza ukeketaji kwa mtoto wa kike.
Elimu
itolewe katika shule za msingi na sekondari kupitia michezo, maigizo ili ujumbe
ufike haraka wamesema vijana hao.
|