Mwenyekiti
wa chama cha Mapinduzi Wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye No3 amekemea
matumizi ya Mitandao ya kijamii kwa wanafunzi katika shule za sekondari bali
wajikite katika masomo ili kufaulu vyema
Hata hivyo
mwenyekiti huyo amezidi kulaani Vikali matumizi ya Madawa ya kulevya kwa
wanafunzi hivyo amewataka wanafunzi hao kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita
matumizi ya madawa ya kulevya mashuleni ikiwemo Bangi pamoja na Viroba.
“Rais Wetu
anapiga vita matumizi ya madawa ya kulevya hivyo tuungane kwa pamoja kwa lengo
la kutokomeza suala hili mshike mwenyezi Mungu katika maisha yenu ili
kufanikiwa” alisema Kiboye.
Hayo
ameyabainisha hii leo alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha Sita
Girango High school iliyopo Wilayani Rorya Mkoani Mara.
|