MKENYA WANJIRU AONYESHA SI MCHEZO KWA KUSHINDA LONDON MARATHON MBELE YA BEKELE WA ETHIOPIA

Mkenya Daniel Wanjiru ameshinda mbio za London Marathon na kumuacha mkali wa mbio hizo, Kenenisa Bekele akichukua nafasi ya pili.
Wanjiru raia wa Kenya ameshinda kwa muda wa saa 2, dakika 5 na sekunde 48 na kuonyesha alikuwa vizuri mbele ya Bekele.
Bekele ndiye anayeshikilia rekodi ya dunia ya mbio za Mita 5000 na 10000 lakini hakuweza mkufua dafu dhidi ya Mkenya huyo.
Kikubwa alichokuwa amelenga Wanjiru ni kuimaliza rekodi ya Mkenya mwenzake, Dennis Kimetto ya 2:02:57  lakini hats hivyo imeshindikana ingawa ameingia kwenye kitabu cha mmoja wa wanariadha bora kabisa kukimbia kwenye London Marathon.
Yeye na Bekele, mwishoni ilikuwa ni ushindani mkali huku Bekele akionyesha kupunguza pengo dhidi yao lakini Mkenya huyo, mwisho alicharuka na kushinda.




Powered by Blogger.