LOGARUSIC NA MWENDO WA MTAJI WA MASIKINI, ATIMULIWA GHANA
Ndiyo
amefikisha miezi mitatu tangu ajiunge na Asante Kotoko ya nchini Ghana,
uongozi wa klabu wa hiyo umemfungashia virago aliyekuwa Kocha Mkuu wa
Simba Mcroatia, Zradvko Logarussic.
Mcroatia
huyo, anatimuwa Asante Kotoko ikiwa ni siku chache tangu mashabiki wa
timu hiyo kumvamia kwenye mazoezi ya timu hiyo kwa kile kilichodaiwa
kupinga mfumo wa 3-5-2.
Kwa
mujibu wa mitandao ya Ghana, matokeo mabaya ya mfululizo waliyoyapata
Asante Kotoko ndiyo sababu ya viongozi kumtimua kocha huyo mwe nye
mbwembwe nyingi.
Viongozi wa Kotoko walifikia maamuzi hayo baada ya kikao cha dhararu kilichofanywa jana Jumapili na viongozi wa timu hiyo.
“Mkataba
wa Zdravko na klabu umevunjwa rasmi na tayari amepewa taarifa rasmi
kutoka kwa uongozi na sasa timu itakuwa chini ya kocha msaidizi, Godwin
Ablordey aatakayekaimu nafasi hiyo hadi hapo tutakapotoa taarifa
nyingine.
"Maamuzi
hayo yametokana na matokeo mabaya ya mfululizo ambayo Katoko
wameyapata kabla ya viongozi kukutana na kujadili mwenendo wa timu
hiyo,"alisema mtoa taarifa huyo.