CAF YAWAPAMBANISHA WALE WALIOIMALIZA YANGA MICHUANO YA AFRIKA
Wwale
wababe waliowaondosha Yanga na Azam kwenye michuano ya Kombe la
Shirikisho Afrika msimu huu, wamekutanishwa kwenye kundi moja katika
michuano hiyo.
Yanga
na Azam ndio waliokuwa wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye michuano ya
kimataifa msimu huu ambapo Yanga ilianzia Ligi ya Mabingwa Afrika,
ilipoondoshwa na Zanaco ya Zambia kwenye hatua ya pili, wakadondokea
Kombe la Shirikisho.
Ikiwa
Kombe la Shirikisho ikaondoshwa na MC Alger ya Algeria, huku Azam
katika michuano hiyo, ilianzia hatua ya pili na kukutana na Mbabane
Swallows ya Swaziland na kuondoshwa kwa jumla ya mabao 3-1.
Katika
ratiba ya hatua ya makundi iliyopangwa juzi Jumatano katika makao makuu
ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) jijini Cairo, Misri, MC Alger na
Mbabane walipangwa Kundi B sambamba na timu za CS Sfaxien ya Tunisia na
Platinum Stars ya Afrika Kusini.
Kundi A: FUS Rabat ya Morocco, Club Africain (Tunisia), Rivers United (Nigeria) na KCCA (Uganda).
Kundi C: Zesco United (Zambia), Recreativo do Libolo (Angola), Al Hilal Elobeid (Sudan) na Smouha (Misri).
Kundi D: TP Mazembe (DR Congo), Supersport United (Afrika Kusini), Horoya AC (Guinea) na CF Mounana (Gabon).