|
|
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds
Media leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt.
Hassan Abbass.
|
 |
|
Katibu wa Kamati ya
Kuchunguza Sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia ofisi za Kituo cha
Televisheni cha Clouds Media, Deodatus Balile akielezea yaliyomo katika ripoti
yao kabla ya kumkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape
Moses Nauye (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam.
|
 |
|
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye (katikati) akifafanua jambo mbele
ya waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu
tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha
Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO
Dkt. Hassan Abbass na Katibu wa Kamati hiyo Deodatus Balile.
|
 |
|
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akikabidhiwa ripoti ya uchunguzi
kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha
Televisheni cha Clouds Media na Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa sakata
hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbass
leo Jijini Dar es Salaam.
|
 |
| Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa tuhuma za
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia kituo cha Televisheni cha
Clouds Media ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan
Abbass (kushoto) akimwelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape
Moses Nnauye ushahidi wa CCTV uliombatanishwa katika CD aliyomkabidhi leo
Jijini Dar es Salaam. |
 |
|
Baadhi ya waandishi
wa habari wakifuatilia makabidhiano ya ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha
Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam.
Picha
zote na: Frank Shija
|
Na Shamimu Nyaki.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amepokea taarifa ya
kina kuhusu chanzo, sababu na namna tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.
Paul Makonda alivovamia kituo cha Utangazaji cha Clouds Media akiwa na walinzi
wenye silaha Machi 17, 2017.
Akipokea
taarifa hiyo leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas ameishukuru Kamati kwa utulivu wao na
kuifanya kazi hiyo kwa utaalamu na umakini mkubwa huku jamii ikitaka matokeo
kwa haraka.
Aidha
Mhe. Waziri amesema kuwa ripoti hiyo ataiwasilisha kwa mamlaka husika kwa ajili
ya uamuzi na maelekezo.
“Nimeipokea
ripoti na ninawahakikishia kuwa nitaikabidhi ripoti hii kwa wakubwa zangu wao
ndo wenye mamalaka ya kufanya chochote”,Alisema Mhe. Nape.
Kamati
aliyoiunda Mhe Waziri ilikuwa na wajumbe wanne ambao ni Bw.Deodatus Balile
kutoka Jamhuri,Bw.Jesse Kwayu wa Gazeti la The Guardian,Bibi Nengida Johanes wa
Upendo Media na Bibi Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
walioongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt.Hassan Abbas .