|
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na
Naibu wa Utangazaji wa Serikali ya
Jamhuri ya Watu wa China Mhe.TONG GANG (katikati waliosimama) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya waandaaji na washiriki wa Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamhiliya
ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo
Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Shamimu Nyaki.
Na Shamimu Nyaki.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
amewaomba Wataalamu wa lugha ya Kichina hapa nchini kutafsiri Filamu za
Kiswahili kwa lugha ya kichina ili zipate soko nchini China.
Prof.
Elisante Ole Gabriel ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa
anazindua Maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” iliyotafsiriwa kwa
lugha ya Kiswahili ambapo amesema kuwa njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwa
watanzania katika filamu za kichina ni kutumia lugha ya Kiswahili.
“Njia
rahisi ya kufikisha ujumbe kwa watu wote
ni kutumia lugha mtambuka katika tamthiliya zetu hii itasaidia sana kukuza uhusiano wetu
na Jamhuri ya Watu wa China”,Alisema Prof.Ole Gabriel.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi vya Luninga Shirika la
Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi Suzan Mungy ameelza kuwa ushirikiano wa shirika
hilo na Kampuni ya Star Times ambayo ndio waandaji wa Tamthiliya hiyo umeleta
mafanikio makubwa ikiwemo kuongezeka kwa
watazamaji wanaopenda tamthiliya za kichina zenye tafsiri ya lugha ya Kiswahili
zinazooneshwa katika luninga hiyo.
“Ushirikiano
wetu unazidi kuimarika na tunaamini utaleta mafanikio makubwa zaidi kwetu sote
katika kutoa elimu na Burudani kupitia Tamthiliya na vipindi vingine vinavyopatikana katika visimbuzi vya Star
Times”,Alisema Bibi Suzan.
Uzinduzi
wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya Kichina “Mfalme Kima” kwa lugha ya
Kiswahili imezinduliwa leo Jijini Dar es Salaam ambapo maudhui yake yanatoa
elimu pamoja na Burudani.
|