Ameyasema
hayo Mjini Dodoma jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada
ya kukutana na kufanya mazungumzo na
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego
kwa mwaliko wa Waziri huyo.
Amesema
kuwa wasanii ni nguzo muhimu katika nchi
sio kwa kufanya kazi ya kuburudisha na
kuelimisha bali katika kuujenga Utamaduni wa nchi ambao ndio nguzo muhimu sana
kwa malezi na makuzi ya wanajamii.
“Niwaombe
wasanii nchini kuzingatia Sheria na taratibu za nchi katika utunzi wao na
utenegenezaji wao wa kazi zao” Alisisitiza Mhe. Dkt Mwakyembe.
Aidha
ameongeza kuwa Serikali haina nia ya kuwanyima uhuru wa kujieleza bali watambue
kuwa nchi inaendeshwa kwa taratibu na Sheria ambazo zinatakiwa zifuatwe na watu
wote.
Kwa
upande wake Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama
Ney wa Mitego amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John
Pombe Magufuli kwa kuwaunga mkono
wasanii nchini na kuahidi kuongeza baadhi ya mambo katika wimbo wake wa “Wapo”
na kuwaalika watanzania kama kuna kero zingine zinazowasumbua katika jamii
wasiwasilishe kwake ili azizungumzie katika wimbo huo.
“Namshukuru
Mhe. Rais kwa kutuunga mkono pia naahidi kufanya “remix” ya wimbo wa “Wapo” kwa
kuongeza maneno niliyoshauriwa na Mhe Rais na Mhe. Waziri na kama kuna mengine
kutoka kwa wananchi pia niko tayari kuyapokea na kuyafanyia kazi” alisema Bw.
Elibariki.
Hivi
karibuni wimbo wa “Wapo” wa Msanii Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego
ulifungiwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kosa la kutozingatia maadili
na baadae kufunguliwa kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
John Pombe Magufuli kupitia Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe.