WANANCHI WAKARIBISHWA KUTEMBELEA VITUO VYA TAARIFA ZA HALI YA HEWA.
|
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya siku ya hali ya
hewa duniani mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Agnes Kijazi.
|
Na:
Frank Shija
WATANZANIA
wamepewa wito wa kutembelea Vituo vya hali ya hewa nchini ili kuona shughuli
zitolewazo na Mamalaka ya Hali ya Hewa
ikiwa ni muendelezo wa kujifunza na kuongeza uelewa juu ya masuala ya
hali ya hewa.
Wito
huo umetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhandisi Edwin Ngonyani wakati akitoa taarifa
kuhusu maadhimisho ya siku ya Hali ya Hewa duniani ambayo inafikia kilele chake
leo tarehe 23 Machi.
“Katika
kuadhimisha siku hii ya hali ya hewa dunia ninatoa wito kwa wananchi kutembelea
katika vituo vya hali ya hewa vilivyopo katika maeneo mengi ya nchi ili waweze
kujifunza zaidi juu ya hali ya hewa na kuongeza uelewa hasa katika elimu juu ya
mawingu,” alisema Mhandisi Ngonyani.
Aliongeza
kuwa katika kuadhimisha siku hiyo mwaka huu
yamejikita katika kuongeza ulewa kwa wananchi kuhusu elimu juu ya
Mawingu ambapo kauli mbiu yake ni, “Tuyaelewe Mawingu na Umuhimu Wake.”
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa(TMA), Dkt. Agness
Kijazi amesema kuwa wananchi ni muhimu kujenga mazoea ya kufuatilia taarifa za
hali ya hewa kwani ni muhimu katika shughuli za maendeleo.
Alisema
maadhimisho ya mwaka huu yamepewa msukumo katika kuongeza uelewa wa wananchi
kuhusu sayansi ya Mawingu na mchango wake katika mzunguko wa maji kati ya nchi
kavu, hali ya hewa ya muda mfupi na mrefu.
Maadhimisho
hayo ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani uadhimishwa tarehe 23 machi kila mwaka yakiusisha
nchi 191 ambazo ni wanachama wa Shirika
la Hali ya Hewa Duniani ikiwa ni moja kukumbuka kuanzishwa kwa Shirika hilo
mnamo mwaka 1950.


