Tumiieni mitandao ya kijamiii kuendeleza injili na maendeleo;
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo |
Washiriki wa kanisa la Waadventista
Wasabato(SDA)wametakiwa kutobaki nyuma katika kutumia mitandao ya kijamii kuendeleza injili na masuala
mengine muhimu kwa ajili ya maendeleo ya jamii .
Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Idara ya
Mawasiliano na IT Divisheni ya Africa Mashariki na Kati(ECD) Mchungaji Steven
Bina wakati wa semina ya
mawasiliano ambayo imeanza leo katika
kanisa la SDA Tarime Central lililopo
Mjini Mkoani Mara.
Mch. Bina amesema kuwa sio dhambi kutumia mitandao
ya kijamii na kusisitza kuwa ina faida nyingi ikitumiwa vizuri.
Semina hiyo ya siku tano imeandaliwa na Idara ya
Mawasiliano Jimbo la Mara( Mara Confrence)) ina lengo la kuhamasisha utumiaji wa mitandao
ya kijamii na vyombo vya habari kusambaza utume wa kanisa , kwa kujibu wa
Mkurugenzi wa Idara hiyo Mchungaji Joseph Matongo.
Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na vyombo vya habari kanisa la SDA Jimbo la Mara Mchungaji Joseph Matongo |
