SIKU YA MAZOEZI YA KILA JUMAMOSI YA PILI YA MWEZI YAFANA UTEGI RORYA.
![]() |
Watumishi wa serikali wakiwemo jeshi la polisi wilayani Rorya Mkoani Mara wakifanya mazoezi |
![]() |
Polisi wakifanya mazoezi |
![]() |
Watatu kushoto ni Mbunge wa jimbo la Rorya Lameck Airo akifuatiwa na Mkurugenzi wa Halamshauri ya wilaya ya Raorya Charles Chacha wakifanya mazoezi. |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Mkurugenzi Rorya Charles Chacha akifanya mazoezi. |
![]() |
![]() |
Picha na kituo cha habari na Mawasiliano Rorya.
Katibu wa michezo wilaya ya rorya Saidi Masanja ambae ni afisa michezo wa wilaya ya rorya amepongeza maamuzi ya serikali kuweka Siku ya mazoezi kitaifa kwani mazoezi ni afya na kusema mazoezi sio kwa watu wanene tu Bali ni kwa watu wote. aliyasema hayo akimkaribisha mwenyekiti wa michezo wilaya ambae ni katibu tawala wa wilaya ya rorya ndg Daudi Murumbe ili aweze kumkaribisha mh mbunge .akimkaribisha mh mbunge mwenyekiti wa michezo amewataka wananchi wawe wanajitokeza kila jumamosi ya pili ya kila mwezi kufanya mazoezi.
amesema mazoezi ni jambo la mhimu kwa magojwa kama malerya na mengine yanayotokana na kutokufanya mazoezi pia akasema michezo ni ajira tofauti na watu wengine wanavyo fikiri.
Mh mbunge amesema mazoezi ni jambo la muhimu sana kwa maisha ya binadamu kwani zoezi hukufanya kuwa na kinga dhidi ya maganjwa ambayo yanatokana na mwili kuwa legelege.akasisitizia jambo la mazoezi kuwa ajenda ya kudumu na kuwa taka wananchi kujitokeza kila inapofika Siku ya mazoezi I'll kuweka afya zetu sawa.
Nae Ocd wa wilaya ya kipolisi ya utegi amesema jeshi la polisi wanao utaratibu wa kila Siku wa kufanya mazoezi.kwao mazoezi ni ajenda ya kudumu ,amewataka wananchi kujiwekea utaratibu wa mazoezi ya kila Siku ili kuweka afya zao salama.
Uzinduzi
Akizindua siku ya mazoezi wilaya ya rorya
Mkuu wa wilaya ya rorya Saimoni Kimori Chacha amepongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi ,wafanyakazi serikalini ,jeshi la polisi,uhamiaji idara ya afya na watu wa kada mbambali.
Pia amempongeza mh mbunge kwa kushiriki na mkurugenzi wa halimashauri pamoja na viongozi wa ccm wa ngazi zote wakiongozwa na katibu wa ccm wilaya ya rorya.mkuu wa wilaya amesema jambo hili ni endelevu kwani ni agizo la serikali kua na Siku ya mazoezi
kitaifa ambayo ni kila Siku ya jumamosi ya pili ya kila mwezi amewataka wananchi wote hususani vijana ambao wengi wao wamekuwa wakiwahi vijiweni na kukaa bila ya kufanya kazi wajiwekee utaratibu WS kufanya kazi.amewataka wananchi kulima mazao yanayo komaa kwa mda mfupi kwa kutumia mvua zinazo nyesha kwa sasa.
Mkurugenzi wa wilaya ya rorya ndg Charles Chacha amewataka wananchi wa rorya kujijengea tabia ya kufanya mazoezi nakusema swala la mazoezi ni jukumu la kila mtu kwa afya yake mwenyewe na siyo jambo la kusukumana inahitaji utayari wa mtu.








