|
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Kushoto) akimkabidhi zawadi
ya Kinyago Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Jamuhuri ya watu wa China Mhe. DONG
WEI (kulia) mara baada ya kusaini Mkataba wa programu ya Utekelezaji wa masuala
ya Utamaduni baina ya Tanzania na China wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi
2020 iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha
na: Genofeva Matemu
Na: Shamimu Nyaki
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na Naibu
Waziri wa Utamaduni kutoka Jamhuri ya watu wa China Mhe. DONG WEI wamesaini programu
ya utekelezaji wa Mkataba wa masuala ya Utamaduni wa miaka mitatu kuanzia mwaka
2017 hadi 2020 leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri
Nape ameeleza kuwa Mkataba huo unalengo la kuimarisha na kuendeleza ushirikiano katika Sekta ya
Utamaduni ambao umedumu kwa miaka mingi ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwl.Julius
K. Nyerere.
“Tanzania
na China tumekuwa na ushirikiano wa muda mrefu wa masuala mbalimbali ikiwemo
hili la Utamaduni ambalo limetumika kukuza, kulinda na kuunganisha nchi zetu
kuwa kitu kimoja”, Alisema Mhe. Waziri.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni wa China Mhe. DONG WEI amesema kuwa
ushirikiano kati ya Tanzania na China uliokuwepo kwa muda mrefu katika masuala ya Utamaduni, Sanaa, Elimu,Ngoma na Michezo yamesaidia kuimarisha ushirikiano
uliopo na kuwezesha nchi hizi mbili kunufaisha katika maeneo hayo.
“Ushirikiano
wetu wa muda mrefu katika masuala ya
Utamaduni umeleta mafanikio makubwa ambayo sote tunajivunia kila tunapokuwa
pamoja”.Alisema Mhe. WEI.
Mkataba
huo pamoja na mambo mengine una lengo la kuendeleza na kufanya mpango wa pamoja
kwa siku za usoni, kufanya matokeo makubwa katika Sekta ya Utamaduni kati ya
nchi hizo mbili, Kufanya mkutano maalum wa ushirikiano wakati muafaka, kuzidisha
ushirikiano kwenye sekta ya viwanda katika bidhaa za Utamaduni na Kubadilishana
wataalamu na mafunzo ya kiutamaduni.
Katika
hatua nyingine Serikali hiyo ya China imeisaidia Wizara kiasi cha Yuan laki nne
(400,000) kwa ajili ya kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya Wizara.
|