Ofisi ya Mbunge Matiko wakabidhi mifuko ya saruji shule ya msingi Buguti Mjini Tarime

Katibu wa Mbunge jimbo la Tarime Mjini Peter Magwi akikabidhi Mifuko 15 ya Saruji  kwa Mwalimu Mkuu msaidizi shule ya Msingi Buguti kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini Esther MatikoCHADEMA  ambayo alihaidi kipindi alipotembelea ujenzi wa shule hiyo mpya ili iweze kujitegemeakwanieneo moja linatumia shule tatu Rebu, Buguti na Mturu.




Ujenzi wa shule ya msingi Buguti iliyopo kata ya Turwa Mjini Tarime inayojengwa kwa nguvu za Wananchi kwa kushirikiana na Mbunge pamoja na Serikali ili kupunguza Wingi wa wanafunzi na suala zima la kusoma kwa zamu.



Kulia ni katibu wa Mbunge Peter Magwi akikabidhi tena mifuko 05  ya Saruji kwa mwenyekiti wa mtaa wa Rebu Shuleni Charles Daniel Kushoto  kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Mtaa huo

Mwenyekiti wa Mtaa wa Rebu Shuleni Charles Daniel Munanka baada ya kupokea Mifuko 05 ya Saruji kutoka kwa Mbunge wa jimbo Tarime Mjini CHADEMA Esther Matiko mwenyekiti huyo amesema kuwa ameamua kujenga ofisi ya mtaa ili kuondokana na kero ya kutunza nyaraka za serikali nyumbani kwake.

 

"Mpaka hapa hili jengo lilipofikia hakuna nguvu za wananchi ni mimi kwa kushirikiana na Mbunge wangu pia hii mifuko mitano aliyotoa pia tulishapokea mifuko mingine mitano na sasa nitaongea na wanachi wangu ili tuchangie suala la maendeleo ili kujenga hii ofisi ya mtaa na itakuwa ofisi ya mfano katika kata zote za mjini "alisema Mwenyekiti.

Powered by Blogger.